Mwanamke mwananchi wa Ujerumani ameuwawa mjini Kabul
ambapo repoti za awali zimedokeza kwamba mauaji hayo yametokea katika
mji huo mkuu wa Afghanistan wakati wa jaribio la utekaji nyara.
Wizara ya mambo ya nje wa Ujerumani imethibitisha kwamba mwanamke wa
Ujerumani ameuwawa wakati wa usiku katika mji mkuu huo mkuu wa
Afghanistan lakini ufafanuzi zaidi kuhusu mauaji hayo haukuweza kufamika
mara moja.Mwanamke huyo hakutajwa jina wala hayakutolewa malezo ya
jinsi alivyouwawa.
Najib Danish naibu msemaji wa wizara ya mambo
ya ndani amesema mwanamke mmoja wa Ujerumani na mlinzi wa usalama wa
Afghanistan wameuwawa wakati mwanamke mmoja wa Finland alitekwa nyara
kutoka nyumba moja ya kulala wageni mjini Kabul wakati wa saa tano na
nusu usiku.
Karolina Romanoff msemaji kutoka wizara ya mambo ya
nje ya Finland amethibitisha kwamba raia mmoja wa Finland ametekwa nyara
lakini hana ufafanuzi zaidil.Wizara ya mambo ya nje imesema katika
taarifa inataka kuachiliwa huru mara moja kwa mtu huyo aliyetekwa nyara.
Scott
Brestlin mfanyakazi wa kampuni yenye makao yake nchini Sweden ya
Opereration Mercy ameliambia shirika la habari la Sweden TT kwamba
mmojawapo wa wafanyakazi wake hajulikani alipo na wameitisha mkutano wa
dharura.
Wajerumani waonywa kutokwenda Afghanistan
Mvulana akiendesha baiskeli mbele ya nyumba alikouwawa mwanamke wa Ujerumani na mlinzi wa Afghanistan.
Wizara
ya mambo ya nje ya Ujerumani imekuwa ikiwaonya watu kwa muda mrefu
kutosafiri kwenda Afghanistan wakati huo huo serikali ya Ujerumani
imekuwa ikishinikiza kuorodheshwa kwa taifa hilo kama taifa salama ili
kuwezesha kurudishwa kwa wakimbizi ambao maombi yao ya kuomba hifadhi
yamekataliwa.
Hakukuwa na taarifa ya mara moja kudai kuhusika
aidha na shambulio hilo au utekaji nyara.Utekaji nyara umekuja kuwa
tatizo kubwa nchini Afghanistan na kwa kawaida huwaathiri wananchi wa
Aghanistan ambao hutekwa nyara kwa ajili ya kudaiwa kulipa fedha za
kuwagombolea.Hata hiyo wageni mara nyingine wamekuwa wakitekwa nyara
nchini humo ili kuzishinkiza serikali zao.
Kabul imekumbwa na
makundi ya uhalifu yalioandaliwa ambayo hupanga utekaji nyara kwa nia ya
kujipatia fedha za ugombozi kwa kuwalenga mara nyingi wageni na raia
matajiri wa nchi hiyo na mara nyengine kuwakabidhi makundi ya waasi.
Hali inazidi kuwa mbaya
Polisi wa Afghanistan wakidumisha usalama Kabul.
Matumizi
ya nguvu yaonyesha hali kuzidi kuwa mbaya nchini Afghanistan ambayo
inakabiliana na uasi wa kundi la Taliban na makundi mengine.
Taliban
imedai kuhusika na mashambulizi yaliyoratibiwa katika kitongoji cha
Shah Joy ilioko katika jimbo la Zabul ambalo ni pigo jengine kwa Jumuiya
ya Kujihami ya NATO ikisaidiwa na vikosi vya Afghanistan.
Asubuhi
ya Jumapili (21.05.2017) kundi la wapiganaji wa Taliban wakiwa na
silaha nzito na nyepesi walifanya mashambulizi hayo ya kuratibiwa kwa
vituo kadhaa vya ukaguzi wa polisi na kuuwa polisi 20.
Gavana wa
jimbo hilo Bismillah Afghamal ameliambia shirika la habari la AFP kwamba
polisi wengine takriban 15 wamejeruhiwa katika mapigano hayo. Shambulio
hilo la karibuni kabisa miongoni mwa mashambulizi ya Taliban
linaonyesha kuongezeka kwa nguu za uasi zaidi ya miaka 15 tokea
walipotimuliwa madarakani na uvamizi wa Marekani hapo mwaka 2001.
No comments:
Post a Comment