Mkutano wa kiuchumi Duniani -World Economic Forum kwa
Afrika umeingia siku yake ya pili hii leo mjini Durban Afrika Kusini,
lengo hasa likiwa kutafuta namna za kukuza uchumi wa Afrika.
Mkutano huo unaokamilika kesho unahudhuriwa na maafisa wakuu
watendaji wa mashirika mbalimbali Afrika, viongozi wa kibiashara, na pia
marais wa zamani na wa sasa barani Afrika.Mkutano huu wa kiuchumi
unafanyika wakati ambapo bara la Afrika linakabiliwa na kiwango cha
juu cha umaskini kuliko ilivyodhaniwa hapo awali, kutokana na miongo
kadhaa ya kufaidi kiuchumi idadi chache ya watu huku mamilioni ya
wengine wakisalia fukara.Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na shirika la
uingereza linalotoa misaada Oxfam upo uwekekano mkubwa katika kipindi
cha miaka mingine 15 ijayo waafrika millioni 250 hadi 350 wakajipata
katika hali mbaya ya kiuchumi kutona na kuendelea kutokuwepo usawa
miongoni mwao.
Hata hivyo baadhi wanahisi hali hii imetokana na usimamizi mbaya wa raslimali za umma na pia kuwepo viongozi wasiowajika swala analokanusha vikali aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano huo wa Durban. Kikwete anasema koloni za mataifa ya Afrika pia kwa kiasi fulani yamechangia kujikokota maendeleo Afrika kwasababu ya kutotoa usadizi wa aiana yeyote ."Ni kweli wakati mwingine kuna matatizo katika utawala lakini tusichukulie kwamba kila kitu ni kutokana na matatizo yalipo kwenye utawala tunapswa kutafakari ukumbwa wa changamoto zilizopo mengi yamekwisha fanywa na mengi yanahitaji kufanywa.Kwa hivyo hizi ni nchi ambazo zinahitaji kusaidiwa."
Rais
huyo wa zamani amesema tayari serikali za mataifa mbalimbali Afrika
zimechukua hatua katika kuboresha elimu katika mataifa yao. Mikakati
hiyo ni pamoja na kuboreshwa elimu kuanzia shule za chekechea,msingi
na hata vyuo vikuu ili kupunguza idadi ya watu wasio na uwezo wa kusoma
na kuandika."Tanzania ilikuwa koloni la ujerumani na vilevile la
Uingereza na mpaka tulipopata uhuru wetu walikuwepo mainjinia wawili
tu.Kwa hivyo tunapokabiliwa na mahitaji makubwa elimu ikiwa miongoni
mwao, utaona matatizo yanajitokeza na hiyo ni kwasababu tulianzia chini
sana na uwekezaji wote huu unaouona katika bara la Afrika umefanyika
baada ya nchi hizi kupata uhuru."
Hata hivyo baadhi wanahisi hali hii imetokana na usimamizi mbaya wa raslimali za umma na pia kuwepo viongozi wasiowajika swala analokanusha vikali aliyekuwa rais wa Tanzania Jakaya Kikwete ambae ni mmoja wa wanaohudhuria mkutano huo wa Durban. Kikwete anasema koloni za mataifa ya Afrika pia kwa kiasi fulani yamechangia kujikokota maendeleo Afrika kwasababu ya kutotoa usadizi wa aiana yeyote ."Ni kweli wakati mwingine kuna matatizo katika utawala lakini tusichukulie kwamba kila kitu ni kutokana na matatizo yalipo kwenye utawala tunapswa kutafakari ukumbwa wa changamoto zilizopo mengi yamekwisha fanywa na mengi yanahitaji kufanywa.Kwa hivyo hizi ni nchi ambazo zinahitaji kusaidiwa."
Msichana mdogo akitafuta mabaki ya chakula katika jaa la taka.
Afrika
na ulimwengu kwa jumla Swaziland ndio nchi inayoongoza katika ukosefu
wa usawa baina ya maskini na matajiri,na kufwatwatiwa kwa karibu na
Nigheria na kisha Afrika kusini ,huku mabillionea watatu wanamiliki
utajiri wa nusu ya idadi ya watu maskini ambayo ni karibu millioni 28.
Mrais wanaohudhuria mkutano huo wa kiuchum mjini Durban ni pamoja na
mwenyeji Jacob Zuma ,Robert Mugabe wa Zimbabwe,Yoweri Museveni wa Uganda
miongoni mwa wengine.Waziri wa fedha hapa ujerumani Wolfgang Schauble
pia anahudhuria mkutano huo.
No comments:
Post a Comment