Makamu wa Rais wa Afrika Kusini ametahadharisha juu ya nchi hiyo kugeuka na kuwa ya Kimafia.
Cyril Ramaphosa
Makamu wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini sambamba na kumkosoa Zuma
amesisitiza kuwa, kama chama tawala wa ANC kinataka kisipoteze himaya na
udhibiti wa jamii ya nchi hiyo, basi hakipaswi kuruhusu Afrika Kusini
igeuke na kuwa nchi ya Kimafia.
Makamu huyo wa Rais wa
Afrika Kusini anayetajwa kama mrithi wa Rais Zuma katika uchaguzi ujao,
ametoa wito wa kuweko uchunguzi huru kuhusiana na faili la ufisadi
ambalo limewatia katika alama ya swali baadhi ya viongozi wa ngazi za
juu wa nchi hiyo.
Chama tawala nchini Afrika Kusini katika miaka ya hivi karibuni
kimepungua umaarufu wake kutokana na viongozi wa ngazi za juu wa chama
hicho akiwemo Rais Jacob Zuma kukabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo
za ufisadi na utovu wa maadili.
Disemba mwaka huu
chama hicho kinatarajiwa kumtangaza mrithi wa Rais Jacob Zuma
anayemaliza muda wake ambapo Cyril Ramaphosa, Makamu wa Rais wa nchi
hiyo amekuwa akitajwa kama chaguo la chama hicho katika uchaguzi ujao
uliopangwa kufanyika nchini humo mwaka 2019.
No comments:
Post a Comment