Tuesday, May 23, 2017

IRAN: MAUAJI YA WAANDAMANAJI BAHRAIN, MATOKEO YA AWALI YA SAFARI YA TRUMP RIYADH

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushambuliwa na kuuawa wananchi wa Bahrain waliokuwa wakishiriki maandamano ya amani ni matokeo ya kwanza ya safari ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Donald Trump nchini Saudi Arabia.
Mohammad Javad Zarif ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: "Hii ni ithibati ya kwanza yenye mashiko kuhusu matokeo ya Rais wa Marekani kuwapongeza madikteta mjini Riyadh. Uvamizi mkubwa dhidi ya waandamanaji yaliyofanywa na utawala wa Bahrain."
Hapo jana askari wa utawala wa Aal-Khalifa nchini Bahrain walivamia eneo la Diraz na kuwashambulia Waislamu wanaomuunga mkono Sheikh Isa Qassim, kiongozi mkubwa wa Waislamu wa Shia, ambapo watu watano waliuawa shahidi huku wengine zaidi ya 280 wakijeruhiwa. 
Polisi wa Bahrain wakiwa katika msako mjini Diraz
Baada ya kutolewa hukumu na mahakama ya nchi hiyo dhidi ya msomi huyo kulikoenda sambamba na kufanyika maadamano ya wananchi katika miji tofauti ya Bahrain jana asubuhi, kwa mara nyingine askari wa nchi hiyo walivamia mji huo na kusababisha machafuko makubwa.
Katika hujuma hiyo askari wa utawala huo wa Aal-Khalifa walivamia makazi ya Ayatullah Isa Qassim na kuwatia mbaroni watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo. 
Wakati huo huo, Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Iran sambamba na kulaani hujuma hiyo amesema uvamizi wa namna hii hautakuwa na tija nyingine ghairi ya kuzidi kuvuga mambo nchini humo na kwamba kushambuliwa watu kwa misingi ya madhehebu zao katu hakuwezi kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Iran

No comments:

Post a Comment