Sunday, May 28, 2017

KOREA KASKAZINI YARUSHA KOMBORA JINGINE KUELEKEA JAPANI

Jaribio hilo limetekelezwa siku moja baada ya taarifa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisimamia jaribio la teknolojia ya kudungua ndege 28 Mei 2017.

Haki miliki ya pichaREUTERS
Image captionJaribio hilo limetekelezwa siku moja baada ya taarifa kwamba kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un alisimamia jaribio la teknolojia ya kudungua ndege za kivita
Korea Kaksazini imerusha kombora la masafa mafupi, ambalo ni la tatu kurushwa na taifa hilo katika kipindi cha wiki tatu.
Kombora hilo aina ya Scud lilipaa umbali wa kilomita 450 (maili 280) kabla ya kuanguka katika maeneo ya bahari ya Japan, hatua iliyoifanya Japan kulalamika vikali.
Wachanganuzi wanasema jaribio hilo ni ishara kwamba Korea Kaskazini inapiga hatua katika kuunda makombora yanayoweza kubeba mabomu.
Korea Kaskazini imeendelea kukiuka azimio la Umoja wa Mataifa linaloizuia kufanya majaribio yoyote ya makombora au silaha za nyuklia, na imeongeza kasi na idadi ya majaribio hayo katika miezi ya karibuni.
Kikosi cha Jeshi la Marekani Bahari ya Pasifiki kimesema kombora hilo lilirushwa kutoka Wonsan, Korea Kaskazini na lilipaa kwa karibu dakika sita kabla ya kuanguka.
Waziri kiranja wa Japan Yoshihide Suga amewaambia wanahabari kwamba kombora hilo lilianguka katika eneo la bahari lililo kati ya visiwa vya Sado na Oki nchini Japan, katika eneo la pamoja la kiuchumi la visiwa hivyo viwili.
Map showing Oki and Sado in Japan, and Wonsan in North Korea
Msemaji wa jeshi la Korea Kusini amesema kombora hilo lilipaa juu hadi kilomita 120 angani, na utathmini unaendelea kubaidi "idadi hasa ya makombora yaliyorushwa," ishara kwamba huenda nchi hiyo ilirusha zaidi ya kombora moja.
Jariibo hilo la kombora limetekelezwa siku moja baada ya vyombo vya habari vya serikali nchini Korea Kaskazini kusema nchi hiyo lilifanyia majaribio mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita, na kutoa picha za kiongozi wa nchi hiyo Kim Jong-un alishuhudia majaribio hayo.
Kim Jong-un.Haki miliki ya pichaAFP/GETTY IMAGES
Image captionKim Jong-un (akiwa na shati la rangi jeupe) anadaiwa kushuhudia kufanyiwa majaribio kwa mfumo mpya wa kudungua ndege za kivita
Korea Kaskazini ina hazina kubwa ya makombora ya masafa mafupi aina ya Scud ambayo yaliundwa na Muungano wa Usovieti.
Makombora ya kisasa ya Scud yanaweza kufika umbali wa kilomita 1,000.
Majaribio mawili ya majuzi yaliyofanywa na Korea Kaskazini, ambayo ilisema yote yalifanikiwa, yalikuwa ya makombora ya masafa ya wastani na masafa marefu.
Korea Kaskazini ilisema jaribio la kwanza lilikuwa la kombora jipya lenye uwezo wa kubeba kichwa cha bomu la nyuklia.
Mifano ya makombora ya Scud yanayomilikiwa na Korea Kaskazini Septemba 5, 2016.Haki miliki ya pichaAFP
Image captionMifano ya makombora ya Scud yanayomilikiwa na Korea Kaskazini
Pyongyang imekuwa ikifanyia majaribio makombora kwa kasi sana, na wataalamu wanasema huenda inakaribia kufanikiwa kumiliki kombora la masafa marefu linaloweza kufikia maeneo ya Marekani bara.
Korea Kaskazini imekuwa ikisema mpango wake wa kustawisha silaha unanuiwa kukabili hatari kutoka kwa uchokozi wa Marekani.
Uwezo wa makombora ya Korea Kaskazini

TRUMP AWAAMBIA WASHAURI MAREKANI KUJITOWA MKATABA WA PARIS

Mtandao wa habari wenye makao yake mjini Washington, Marekani umeripoti kwamba Rais Donald Trump amewaambia "watu anaowamini" ataachana na makubaliano ya kihistoria ya tabia nchi yaliofikiwa Paris Ufaransa.

China | Illegale Stahlfabriken unterlaufen Chinas Emissionsgesetze (Getty Images/K. Frayer)
Mtandao wa habari wenye makao yake mjini Washington nchini Marekani umeripoti kwamba Rais Donald Trump wa Marekani amewaambia "watu anaowamini" ataachana na makubaliano ya kihistoria ya tabia nchi yaliofikiwa Paris Ufaransa ambayo mtangulizi wake Barack Obama ameyasaini hapo mwaka 2016 kupunguza kiwango cha utowaji wa hewa ukaa gesi yenye kuchafuwa mazingira duniani.
Kutokuwepo kwa hali ya uhakika kuhusiana na msimamo wa Marekani juu ya suala la tabia nchi kumewatibuwa viongozi wenzake katika mkutano wa kilele wa nchi za G7 zenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani ambao umemalizika Jumamosi huko Taormina, Sicily nchini Italia bila ya kuwepo kwa maafikiano ya sauti moja kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Rais Donald Trump amesema atotowa uamuzi wa mwisho wiki hii iwapo Marekani iendelee kubakia katika makubaliano ya tabia nchi yaliyofikiwa Paris au ijitowe. Trump ametowa tangazo hilo la ghafla katika mtandao wa Twitter baada ya kuhimili shinikizo kutoka kwa viongozi wa Ulaya waliokuwa wakimtaka abakie katika mkubaliano hayo.
Vyanzo vya kuaminika
G7 Gipfeltreffen Donald Trump spricht mit Angela Merkel und Beji Caid Essebsi (Reuters/J. Ernst)
Viongozi wa nchi za G7 katika mazungumzo.
Ikitaja vyanzo vitatu vyenye uwelewa wa moja kwa moja wa mipango ya Trump ukurasa wa kutowa habari wenye kuheshimika Axios umeripoti Jumamosi kwamba kiongozi huyo wa Marekani amewaambia washauri wake wakuu ataitowa Marekani kwenye makubaliano ya tabia nchi yaliofikiwa Paris mwaka 2015.
Ukurasa huo umeanzishwa mwaka jana na mmojawapo wa wasisi wenza wa kisiasa na mkuu wa zamani wa waandihishi  wa Ukulu ya White House.Ukurasa huo wa Axios umesema iwapo ni kweli utabiruwa sera za tabia nchi za mtangulizi wake Barack Obama na kutuma ishara ya mapambano kwa dunia nzima kwamba suala la kuongezeka kiwango cha joto duniani si miongoni mwa vipau mbele vya Trump.
Ukurasa huo wa mtandao umekiri kwamba rais huyo tajiri mkubwa kabisa amebadili mawazo yake juu ya ahadi kadhaa madhubuti alizotowa wakati wa kampeni tokea aingie madarakani hapo mwezi wa Januari.
Uamuzi wiki hii
G7 Gipfeltreffen in Taormina Italien US-Präsident Donald Trump (Reuters/D. Martinez)
Rais Donald Trump wa Marekani.
Trump amewaambia viongozi katika mkutano wa G7 kundi la mataifa lenye maendeleo makubwa ya viwanda duniani huko Italia hapo Jumamosi(27.05.2017) kwamba atatowa uamuzi wake kuhusu iwapo Marekani iendelee kuunga mkono makubaliano ya kihistoria ya tabia nchi katika kipindi kisichozidi wiki moja.Nchi za kundi la G7 zinajumuisha miongoni mwa nchi nyengine Ujerumani,Uingereza,Canada,Ufaransa na Japani.
"Nitatowa uamuzi wa mwisho juu ya mkataba wa Paris wiki ijayo!" ameandika Trump kwenye mtandao wa Twitter bada ya huko nyuma kuita ongezeko la joto duniani kuwa ni "dhihaka".
Ukosefu wa kujitolea wa Trump kwa makubaliano hayo ya tabia nhi ambayo yanazitaka nchi kujifunga kupunguza kiwango kikubwa sana cha utowaji wa hewa ukaa kupunguza madhara ya kuongezeka kiwango cha ujoto duniani kumewatibuwa washirika wa jadi wa Marekani ikiwemo Ujerumani.
Kansela Angela Merkel wa Ujerumani amesema mazungumzo ya G7 kuhusu tabia nchi yamekuwa na matatizo magumu sana.Amewaambia waandishi wa habari majadiliano kuhusu tabia nchi yalikuwa magumu sana na kama sio kusema hayaridhishi kabisa" na kwamba "hakuna dalili iwapo Marekani itabakia katika makubaliano ya Paris au hapana."
Mkubaliano hayo ya kihistoria ya tabia nchi yalisainiwa na nchi 195 mjini Paris hapo mwezi wa Disemba mwaka 2016 na kuanza kufanya kazi miezi 11 baadae.Mkataba huo umezifunga nchi kuzuwiya kuongezeka kwa ujoto kupindukia nyuzi joto mbili kiwango kilichokuweo kabla ya enzi za viwanda.

WATAALAMU WA UN WALAANI SAUDIA KUBOMOA TURATHI ZA KIUTAMADUNI ZA MJI WA KISHIA

Wataalamu wa Umoja wa Mataifa wameulaani utawala wa Saudi Arabia kwa kubomoa turathi za mji wa kale wa Waislamu wa madhehebu ya Shia mashariki mwa nchi hiyo.
Katika taarifa, Karima Bennoune Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya haki za kiutamaduni amesema hatua ya Saudia kubomoa eneo la kale la mji wa Awamyah linalojulikana kama al Masourah ni ukiukwaji wa haki za binadamu. Amesema watawala wa Saudia wamebomoa turathi hiyo ya kiutamaduni pamoja na kuwa walikuwa wametakiwa na Umoja wa Mataifa kutofanya hivyo.
Katika taarifa iliyotolewa kupitia Ofisi  ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, Bennoune amesema vikosi vya usalama vya Saudia vimeharibu kabisa majengo ya kihistoria na kuwalazimisha wakaazi kukimbia eneo hilo.
"Uharibifu huu unafuta kabisa historia na turathi ya utamaduni na ni ukiukwaji wa wazi wa majukumu ya Saudia kwa mujibu wa sheria za kimataifa za haki za binadamu," amesema afisa huyo wa Umoja wa Mataifa,
Vifaru vya Saudia vinatumika kuwahujumu raia wa nchi hiyo
Baadhi ya majengo ya eneo hilo yanaripotiwa kujengwa zaidi ya miaka 400 iliyopita. Kwa upande wake Leilani Farha, Ripota Maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya makazi bora ameonya kuwa hatua hiyo ya Saudia kubomoa makaazi ya kale ya Waislamu wa madhehebu ya Shia inahesabiwa kuwa, 'ufurushaji wa lazima katika sheria za kimataifa za haki za binadamu"
Mnamo Mei 10, watu wawili waliuawa wakati wanajeshi wa Saudia walipovamia eneo la al Masourah na kubomoa nyumba za kale katika eneo hilo.
Watawala wa Saudia wamekiharibu kijiji cha al-Masourah ambako ndiko alikozaliwa Sheikh Nimri Baqir an-Nimr, mwanazuoni mkubwa wa Waislamu wa Kishia aliyeuawa kwa kukatwa kichwa na utawala huo mwaka jana. Watawala hao wa Saudia walikibomoa kijiji hicho kwa madai ya eti kukiboresha.
Kijiji cha al-Masourah kinafahamika kama nembo ya malalamiko huko mashariki mwa Saudia dhidi ya watawala wa nchi hiyo ya kidikteta.

KUMALIZIKA SAFARI YA RAIS WA MAREKANI BARANI ULAYA BILA YA KUFIKIA MAKUBALIANO


Rais Donald Trump wa Marekani amemaliza safari yake ya mara ya kwanza barani Ulaya tangu aingie madarakani; bila ya kufikia natija iliyotarajiwa.
Katika duru ya safari hii, Trump alikutana na viongozi wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) mjini Brussels, Ubelgiji na kadhalika viongozi wa nchi wanachama wa kundi la G7 mjini Sicily, Italia. Kadhalika Trump kwa mara ya kwanza alifika Vatican na kukutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis ambapo pia alifanya naye mazungumzo. Katika vikao na mikutano hiyo kulijadiliwa masuala ya biashara, mabadiliko ya hali ya hewa, njia za kukabiliana na ugaidi na matokeo ya wimbi la wahajiri wanaoelekea barani Ulaya. Pamoja na hayo katika maudhui zote hizo kuliwabainikia walimwengu mpasuko wa mtazamo kati ya Marekani na waitifaki wake.
Trump alipokutana na Kiongozi wa Kanisa Katoliki Duniani Papa Francis
Katika suala la biashara, kundi la G7 kwa mara nyingine na kinyume na mtazamo wa Marekani, lilikosoa vikali sera za kiuchumi za Washington. Hata hivyo kundi hilo chini ya mashinikizo ya kamati ya Marekani kwa uongozi wa Trump mwenyewe, lilikubali katika kikao cha mjini Sicily, Italia kwamba vifungu vya ukosoaji wa kibiashara visivyo vya kiuadilifu, lazima viwekewe masharti maalumu. Kabla ya hapo viongozi wa Marekani walionyesha matumaini yao kwamba katika kikao cha kwanza cha viongozi wa kundi la G7 pamoja na Rais Donald Trump, muungano huo muhimu wa kiuchumi, ungeunga mkono sera za kiuchumi za Marekani. 
Kabla ya kikao kuanza huko mjini Sicily, Italia
Hata hivyo nchi kama vile Ujerumani, Japan, Ufaransa na Canada ambazo zinastawi katika uzalishaji na ambazo zimewekeza katika uzalishaji wa bidhaa kwenda masoko yenye watumiaji wengi ya Marekani, zilipinga madai ya kila siku ya Washington ya 'Marekani Kwanza.' Ama kuhusiana na suala la mabadiliko ya hali ya hewa pia viongozi wa kundi la G7 hawakuweza kufikia makubaliano na rais huyo wa Marekani. Hii ni kwa kuwa nchi za Ulaya za muungano huo zililipa kipaumbele suala la kuandaliwa na kutekelezwa mikataba ya kimataifa kwa ajili ya kukabiliana na mabadiliko ya hali ya hewa, katika hali ambayo Trump aliahidi kuitoa nchi yake katika mkataba huo uliofikiwa mjini Paris, Ufaransa. Washirika wa Marekani katika kundi la G7 au katika Umoja wa Ulaya wana wasiwasi mkubwa endapo Marekani ambayo ndiyo nchi inayoharibu zaidi hali ya hewa duniani, itajitoa katika mkataba huo wa mjini Paris.
Viongozi wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO)
Inatabiriwa kuwa, tangazo la Washington la kujitoa katika mkataba huo, litatoa pigo jingine kwenye mahusiano yake na nchi za Ulaya na Asia. Mbali na kundi la G7, katika kikao na viongozi wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO) mjini Brussels, Ubelgiji pia, Rais Donald Trump wa Marekani hakuweza kupata kile alichokuwa amekitarajia tangu awali. Kabla ya kikao hicho viongozi wa ngazi ya juu wa serikali ya Marekani walikuwa wametangaza kuwa, wana matumaini nchi wanachama katika muungano huo zitakubaliana na pendekezo la kuongezwa bajeti na kujiunga katika muungano wa eti kupambana na Daesh (ISIS). Kinyume kabisa na na matarajio ya Washington, hakuna kauli yoyote iliyotolewa katika kikao cha mjini Brussels, Ubelgiji ya kuunga mkono pendekezo hilo la Marekani.
Kikao cha viongozi wa kundi la Saba
Hii ni katika hali ambayo ilikuwa imepangwa baadhi ya nchi wanachama wa NATO ziongeze pesa zaidi za mchango kwa ajili ya masuala ya kiulinzi. Aidha katika suala la vita dhidi ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh (ISIS) nchi wanachama wa Muungano wa Kijeshi wa Nchi za Magharibi (NATO), zilikubali tu kuunga mkono kilojestiki operesheni za muungano unaoongozwa na Marekani wa eti kupambana na Daesh. Hii ni katika hali NATO imetangaza rasmi kutoshiriki katika vita hivyo vya Daesh katika maeneo ya magharibi na kaskazini mwa Asia. Inaonekana wazi kuwa wasiwasi wa matokeo ya kiusalama na kisiasa katika vita vyao na kundi la Daesh, ndiyo sababu kuu ya nchi wanachama wa muungano huo wa kijeshi kutupilia mbali pendekezo la Marekani. Alaa kulli hal, msimamo wa miungano miwili ya NATO na kundi la G7 katika kupambana na ugaidi, imemfanya Donald Trump kushindwa kupata alichokitaka kutoka kwa washirika wake wakubwa. Inatazamiwa kuwa kushindwa huko kwa Washington kulikotokana na faili linalohusiana na uhusiano wa Trump na Russia kutaongeza mashinikizo ambayo hata hivi sasa si machache, dhidi ya serikali ya Marekani na Trump mwenyewe.

47 WAUAWA KATIKA MAPIGANO KATI YA MAKUNDI HASIMU LIBYA

Kwa akali watu 47 wameuawa katika mapigano yanayoendelea katika mji mkuu wa Libya, Tripoli, kati ya wapiganaji wa makundi mawii hasimu ya kisiasa.
Wizara ya Afya ya Libya imesema mbali na mauaji hayo, watu wengine zaidi ya 180 wamejeruhiwa, huku idadi ya raia miongoni mwa wahanga hao ikikosa kujulikana.
Mapigano hayo yalianza Ijumaa iliyopita, na kushtadi hapo jana hususan katika wilaya za Abu Salim, Salahedeen, na Qasr Bin Ghashthen.
Wapiganaji wa serikali ya Libya inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa hata hivyo imesema imepoteza wapiganaji 52 katika mapigano ya jana Jumamosi.
Martin Kobler, Mjumbe Maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Libya amelaani vikali mauaji hayo na kuzitaka pande zote kukomesha uhasama, kulinda raia na kushirikiana kufikia utangamano wa kitaifa.
Mbali na mapigano ya pande mbili hasimu, genge la Daesh pia limevuruga usalama Libya
Siku 10 zilizopita, watu zaidi ya 100 waliuawa katika mapigano mengine kati ya makundi hayo hasimu, yaliyofanyika baada ya kikosi cha jeshi kutoka mji wa magharibi mwa Misrata kuvamia kituo cha jeshi kilichoko katika mji wa Brak Al-Shati.
Mapigano hayo yanajiri katika hali ambayo, mapema mwezi huu, Khalifa Haftar, Mkuu wa Jeshi la Libya mashariki mwa nchi hiyo na Fayez al Sarraj, Waziri Mkuu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya walikutana mjini Abu Dhabi, Imarati na kufikia makubaliano kuhusu utatuzi wa hitilafu za pande hizo mbili. Viongozi hao wawili walikubaliana pia kuunda jeshi moja na kusimamia kwa pamoja uchaguzi wa Rais na Bunge katika kipindi cha miezi sita ijayo.

WANAJESHI WA YEMEN WALIPIZA KISASI KWA KUUA ASKARI 13 WA SAUDIA

Wanajeshi wa Yemen wametekeleza oparesheni kubwa ya kulipiza kisasi na kuuawa wanajeshi 13 Wasaudi katika maeneo kadhaa ya kusini magharibi mwa Saudi Arabia.
Askari sita kati ya waliouawa walikuwa katika kituo cha kijeshi cha Al Fuaz katika eneo la Najran nchini Saudi Arabia.
Wanajeshi wa Yemen pia wameshambulia gari la deraya na kuangamiza askari watatu Wasaudi waliokuwa katika kituo cha kijeshi cha Alib eneo la Asir. Wanajeshi wengine wanne Wasaudi waliuawa katika eneo lililo karibu na hilo. Askari wa Jeshi la Yemen wakishirikiana na wapiganaji wa Ansarullah wamekuwa wakiilinda nchi hiyo ambayo ilivamiwa na Saudi Arabia Machi 2015.
Wapiganaji wa Ansarullah
Saudia iliivamia Yemen kwa himya ya Marekani kwa lengo la kuirejesha madarakani serikali kibaraka ya Abdu Rabuh Mansour Hadi aliyejiuzulu na kukimbilia mji mkuu wa Saudia, Riyadh.
Raia zaidi ya elfu 12  wa Yemen wameuawa na maelfu ya wengine kujeruhiwa katika uvamizi huo wa kijeshi huku Umoja wa Mataifa ukishindwa kuchukua hatua yoyote ya kuzuia jinai hizo za Saudia huko Yemen. 

Tuesday, May 23, 2017

CHAMA TAWALA AFRIKA KUSINI CHAKANUSHA RIPOTI ZA KUJADILI KUMUONDOA MADARAKANI RAISI ZUMA

Chama tawala nchini Afrika Kusini ANC kimezitioa maanani na kueleza kuwa hazina ukweli ripoti za vyombo vya habari kwamba suala la kumwondoa madarakani Rais wa nchi hiyo Jacb Zuma litajadiliwa katika mkutano muhimu wa chama hicho utakaofanyika mwishoni mwa wiki.
Msemaji wa ANC Zizi Kodwa amekanusha ripoti hizo akisistiza kuwa ni za "kutunga na hazina ukweli".
Upinzani dhidi ya Zuma ndani ya chama tawala na kutoka vyama vya upinzani pamoja na makundi ya asasi za kijamii umeongezeka tangu kiongozi huyo alipomuuzulu waziri wa fedha anayeheshimika Pravin Gordhan mwezi Machi mwaka huu, hatua ambayo ilisababisha kushuka itibari ya kiuchumi ya Afrika Kusini.
Shirika la habari la Bloomberg limezinukuu duru mbili zikiripoti kuwa  ANC itajadili suala la kumwondoa madarakani Rais Zuma katika mkutano wa viongozi wa juu wa chama hicho utakaofanyika mwishoni mwa wiki, ripoti ambazo zimesababisha thamani ya sarafu ya nchi hiyo ya randi kupanda kwa asilimia 1.5 dhidi ya dola.
Pravin Gordhan
Rais Jacob Zuma, mwenye umri wa miaka 75, ambaye kipindi chake cha uongozi kinamalizika mwaka 2019, alinusurika na jaribio la ndani ya chama la kumwondoa madarakani mwaka 2016 baada ya Mahakama ya Katiba kutoa uamuzi kwamba alikiuka kiapo cha urais kwa kukataa kurejesha serikalini malipo ya fedha alizotumia kuboresha nyumba yake binafsi.
Zuma alihusishwa pia kwenye ripoti ya taasisi ya kupambana na ufisadi na tuhuma za kuruhusu jamaa wa familia moja ya wafanyabiashara wazaliwa wa India kuwa na ushawishi katika uteuzi wake wa baraza la mawaziri na katika zabuni zinazotolewa na makampuni ya serikali.
Hata hivyo kiongozi huyo na familia hiyo ya Gupta wamekanusha kutenda kosa lolote lile.../

IRAN: MAUAJI YA WAANDAMANAJI BAHRAIN, MATOKEO YA AWALI YA SAFARI YA TRUMP RIYADH

Waziri wa Mambo ya Nje wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema kushambuliwa na kuuawa wananchi wa Bahrain waliokuwa wakishiriki maandamano ya amani ni matokeo ya kwanza ya safari ya hivi karibuni ya Rais wa Marekani, Donald Trump nchini Saudi Arabia.
Mohammad Javad Zarif ameandika katika ukurasa wake wa Twitter kuwa: "Hii ni ithibati ya kwanza yenye mashiko kuhusu matokeo ya Rais wa Marekani kuwapongeza madikteta mjini Riyadh. Uvamizi mkubwa dhidi ya waandamanaji yaliyofanywa na utawala wa Bahrain."
Hapo jana askari wa utawala wa Aal-Khalifa nchini Bahrain walivamia eneo la Diraz na kuwashambulia Waislamu wanaomuunga mkono Sheikh Isa Qassim, kiongozi mkubwa wa Waislamu wa Shia, ambapo watu watano waliuawa shahidi huku wengine zaidi ya 280 wakijeruhiwa. 
Polisi wa Bahrain wakiwa katika msako mjini Diraz
Baada ya kutolewa hukumu na mahakama ya nchi hiyo dhidi ya msomi huyo kulikoenda sambamba na kufanyika maadamano ya wananchi katika miji tofauti ya Bahrain jana asubuhi, kwa mara nyingine askari wa nchi hiyo walivamia mji huo na kusababisha machafuko makubwa.
Katika hujuma hiyo askari wa utawala huo wa Aal-Khalifa walivamia makazi ya Ayatullah Isa Qassim na kuwatia mbaroni watu waliokuwa ndani ya nyumba hiyo. 
Wakati huo huo, Bahram Qassemi, Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Iran sambamba na kulaani hujuma hiyo amesema uvamizi wa namna hii hautakuwa na tija nyingine ghairi ya kuzidi kuvuga mambo nchini humo na kwamba kushambuliwa watu kwa misingi ya madhehebu zao katu hakuwezi kuupatia ufumbuzi mgogoro uliopo.
Msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Iran

MUIGIZAJI WA JAMES BOND ROGER MOORE AFARIKI DUNIA

Roger Moore nyota wa filamu alieigiza kwa muda mrefu zaidi kama James Bond, amefariki nchini Uswisi kwa maradhi ya Saratani akiwa na miaka 89.

Roger Moore Maud Adams Britt Eklund Der Mann mit dem goldenen Colt (picture-alliance/dpa)
Roger Moore hakuwa mtu aliejigamba kuhusu uwezo wake wa kuigiza lakini ukweli ulijidhihirisha wenyewe -- aliigiza kama James Bond katika filamu nyingi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Akijulikana kwa nyusi zake zilizopanda juu kiajabu na stihizai zisizoonyesha hisia, mtazamano wa Moore kuhusu jasusi huyo wa juu alikuwa mcheshi zaidi kuliko mtangulizi wake Sean Conery.
Lakini alimpiku Conery na waigizaji wote waliowahi kuigiza 007 kwa kuigiza nafasi aliopendelea kuiita "Jimmy Bond" katika rekodi ya filamu saba. Moore pia alikuwa wa mwisho miongoni mwa nyota wa filamu wa mfumo wa kizamani, aliewahesabu Frank Sinatra na David Niven miongoni mwa marafiki zake na aliishi maisha ya anasa nchini Uswisi na kwenye pwani ya Meditrannia ya kusini-masahriki mwa Ufaransa.
Aliendelea kuwa shujaa wa maisha halisi na balozi wa shirika la UNICEF hata wakati akipuuza vipaji vya mwenyewe. "Mimi siyo aina ya muuaji ya kinyama. Ndiyo maanda naigiza nafasi hiyo zaidi kwa kuchekesha," aliwahi kunukuliwa akisema.
James Bond 007 Moonraker (picture-alliance/KPA)
Roger Moore katika filamu ya "Moonraker" akiwa na Lois Chiles alieigiza kama Holly Goodhead na Richard Kiel alieigiza kama Jaws.
Mwanzo wa kazi ya uigizaji
Roger George Moore alizaliwa Oktoba 14, 1927 katikakiunga cha jiji la London cha Stockwell, akiwa mtoto pekee wa afisa wa polisi mwenye cheo cha constable na mke wake, na alikulia katika maisha mazuri. " Sikuwa na maisha mabaya kama mvulana kutoka Stockwell, ambako nilikuwa naangalia cinema kwa mshangao, bila kujua kwamba ningekuwa sehemu ya ulimwengu huu wa ajabu," aliandika katika wasifu wake," Uliwengu wangu ni Bond wangu."
Moore alianza kazi ya uingizaji kama msaidizi katika miaka ya 1940 kabla ya kusoma katika chuo cha kifalme cha masomo ya sanaa ya maigizo. Alipata mkataba wa studio za MGM lakini alikuwa tu na jukumu la usaidizi katika miaka 1950. Ilikuwa ni katik muongo uliofuata ambapo alipata umaarufu duniani, akiigiza katika kipindi cha televisheni cha Uingereza "The Saint" kama  Simon Templer, mpenda vituko mwenye kujisifu.
Moore alisema katika wasifu wake kwamba aliwahi kuombwa kuigiza James Bond mwaka 1967. Lakini ilikuwa mwaka 1973 ambapo alipata nafasi hiyo -- licha ya kuwa kwa umri wa miaka 45, alikuwa mkubwa kwa mwaka mmoja na nusu zaidi yaConnery, mtu aliemrithi katika nafasi hiyo.
Roger Moore Tanya Roberts Im Angesicht des Todes (picture-alliance/dpa/Goldschmidt)
Roger katika kipande cha filamu ya "View to a Kill" ya mwaka 1985 akiwa na "Bond Girl" Tanya Roberts.
Moore aliigiza mara ya kwanza katika filamu ya "Live and Let Live", baaday a watengenezaji kumfanya aüunguze uzito, kuwa fiti na kukata nywele zake. Alifuatia filamu hiyo na "The Man With the Golden Gun" (1974), "The Spy Who Loved Me" (1977), "Moonraker" (1979), "For Your Eyes Only" (1981) na "Octopussy" (1983) kabla ya kutupa daruga baada ya kuigiza "A View to a Kill" mwaka 1985, akiwa na umri wa miaka 57.
Moore alisema filamu ya Bond alioifurahia zaidi ni "The Spy Who Loved Me", inayokumbukwa kwa kuhusisha nafasi kadhaa za uhalifu zilizohusisha mfano "Jaws" ilioigizwa na Richard Kiel -- aliefariki 2014, na vifaa vikiwemo gari la mashindano la Lotus Esprit, ambalo lilitumika vilevile kama nyambizi.
"Nadhani 'The Spy Who Loved Me' ndiyo ilikuwa bora, au kwa meneno mengine nilioifurahia zaidi," Moore aliliambia shirika la habari la Ufaransa AFP katika mahojiano kwa njia ya barua pepe mwaka 2007. "Ilikuwa na maeneo mazuri. Na nilifurahia kupita kiasi kufanya kazi na mkurugenzi Lewis Gilbert.
Moore aliigiza katika filamu nyingine wakati na baada ya miaka ya Bond lakini hakuna kati ya hizo filamu nyingine iliokuwa na mafanikio kama ya 007. Moore pia alifurahi maisha ya hali ya juu, akiwa na kundi la nyota na majumba kusinimagharibi mwa Uswisi na Monaco.
Balozi wa hisani wa UNICEF
Lakini katika miaka ya karibuni Moore alijulikana kwa kazi zake za kiutu, kupitia shughuli kama balozi wa hisani wa UNICEF, akisaidia kukusanya feza kwa ajili ya watoto wanaoishi katika maisha magumu. Alipewa hadhi ya shujaa wa ukoo bora mwaka 2003 katika kutambua kazi yake na shirika hilo.
UK Roger Moore (picture alliance/dpa/R. Vennenbernd)
Roger Moore alivyoonekana katika picha hii iliochukuliwa 25.06.2013 kabla ya kufanyiwa mahojiano mjini Aachen, na shirika la habari la Ujerumani dpa.
Mwaka 1993 alifanyiwa upasuaji wa saratani ya tezi dume, mwaka 2003 aliwekewa kifaa cha mapigo ya moyo "pacemaker" na 2013 aligunduliwa kuwa na ugonjwa wa kisukari. Mwaka 2014 alichapisha kitabu chake cha "Last Man Standing: Tales from Tinseltown" kilichopewa kichwa cha "One Lucky Bastard" nchini Marekani. Mwaka 2015 alishika nambari 38 katika jarida la Uingereza la GQ miongoni mwa wanaume wanaopendeza zaidi kimavazi.
Moore aliowa mara nne na ameacha watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike. Watoto wake wote aliwazaa na muigizaji wa Kitaliano Luisa Mattioli, aliemuoa mwaka 1969 na kumtaliki 1996. Kisha alimuoa Msweden Kristina Tholstrup mwaka 2002.

WAISLAMU KENYA: SERIKALI YA JUBILEE ISITUMIE SUALA LA UHURU WA RAMADHANI KATIKA KAMPENI, NI HAKI YA KILA MKENYA

Shakhsia mbalimbali wa Kiislamu nchini Kenya, wameitaka serikali kuwahakikishia Waislamu usalama wa kutosha ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani baada ya serikali hiyo kuondoa hali ya hatari katika maeneo ya mpakani na Somalia.
Viongozi hao wa Kiislamu wameionya serikali kutumia suala hilo kwa ajili ya kujisafisha katika kampeni za uchaguzi, huku wakisisitiza kuwa, uhuru wa kufanya ibada na uhuru kwa ujumla ni haki ya kila Mkenya na sio zawadi.
Vijana waliouawa Mandera, Kenya kwa kuhusishwa na genge la ash-Shabab
Maeneo ya mpakani mwa Kenya na Somalia yamekuwa katika hali ya hatari kwa muda wa miezi kadhaa sasa tangu mwishoni mwa mwaka jana.
Tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Mombasa Seifullah Murtadha kwa taarifa kamili………../
Magaidi wanaodhaniwa kuwa wanachama wa ash-Shabab

MALALAMIKO YA WAYEMEN KWA KIGUGUMIZI CHA UMOJA WA MATAIFA

Wakazi wa mji mkuu wa Yemen Sana'a wamefanya maandamano sambamba na safari ya Ismail Ould Sheikh Ahmad, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen mjini humo na kutaka kuhitimishwa mzingiro wa pande zote dhidi ya nchi hiyo.
Waandamanaji hao wakiwa wamebeba mabango na maberamu wamelaani vikali kimya cha kutia aibu cha Umoja wa Mataifa mkabala na matatizo na masaibu ya wananchi wa Yemen na hatua ya umoja huo ya kutochukua hatua za kivitendo katika uwanja huo. Ismail Ould Sheikh Ahmad, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen Jumatatu ya jana aliwasili mjini Sana'a kwa shabaha ya kukutana na makundi ya nchi hiyo lengo likiwa ni kuandaa mazingira ya kufanyika duru mpya ya mazungumzo ya amani ya Yemen.
Katika mazingira kama haya, msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen ametangaza kuwa, madhali Umoja wa Mataifa hauna uwezo wa kufanya chochote, kukutana na wawakilishi wa umoja huo ni hatua isiyo na maana wala faida yoyote. Isipokuwa kama Umoja wa Mataifa utabadilika na kufungamana na ubinadamu, maadili na kufanya kazi kwa mujibu wa majukumu yake. Muhammad Abdul-Salam, msemaji wa Harakati ya Ansarullah ya Yemen alitangaza hapo jana kwamba, tajiriba inaonyesha kuwa, Umoja wa Mataifa huchukua hatua pale madola makubwa yanapotaka umoja huo uchukue hatua. Abdul-Salam ameongeza kuwa, wananchi wa Yemen wanakabiliwa na hali mbaya ya kibinadamu hivi sasa lakini Umoja wa Mataifa umefumbia macho hilo.
Ndege za kijeshi za Saudia huishambulia Yemen kila siku
Saudia ikipata himaya ya Marekani ilianzisha hujuma dhidi ya Yemen mwezi Machi mwaka 2015 kwa lengo la kumrejesha madarakani kibaraka wake Abdrabbuh Mansur Hadi, rais wa zamani wa Yemen aliyejiuzulu nafasi hiyo na kutoroka nchi. Kwa kuzingatia faili la utendaji dhaifu wa Umoja wa Mataifa katika kutatua migogoro mbalimbali ulimwenguni si ajabu kuona umoja huo ukiathirika na lobi za Wasaudia na kubadilisha misimamo yake badala ya kutekeleza majukumu yake ipasavyo na kuwa upande wa wananchi wanaotaabika wa Yemen. Ni katika mazingira haya ndipo Ban Ki-moon, Katibu Mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa akaitoa Saudia katika orodha nyeusi ya nchi zinazofanya mauaji dhidi ya watoto, hatua ambayo ilifuatiwa na maswali mengi hasa kutokana na kuwa wadhiha jinai za Aal Saud dhidi ya watoto wa Yemen.
Kigugumizi cha Umoja wa Mataifa mkabala na mauaji ya umati dhidi ya wananchi wa Yemen yanayofanywa na utawala wa Aal Saud na mamluki wake linahesabiwa kuwa jambo hatari mno ambalo kimsingi linakinzana bayana na majukumu na malengo ya umoja huo. Hatua hizo za Umoja wa Mataifa zimeifanya taasisi hiyo ya kimataifa ihesabiwe kuwa mshirika wa jinai za Saudia huko Yemen. Kwa mwenendo huo, Umoja wa Mataifa haujakuwa na utendaji unaotakiwa mkabala na mgogoro wa Yemen na kwa msingi huo haujaweza kuzuia jinai za utawala wa Aal Saud huko Yemen.
Antonio Guterres, Katibu Mkuu mpya wa Umoja wa Mataifa
Wachambuzi wa mambo wanaamini kuwa, hatua pekee iliyochukuliwa na Umoja wa Mataifa na ambayo inatazamwa kwa jicho zuri na walimwengu ni juhudi za mwakilishi wake maalumu katika masuala ya Yemen za kuitisha mazungumzo ya kitaifa, hatua ambayo nayo haikuweza kufunika kigugumizi cha umoja huo katika mgogoro wa nchi hiyo. Hata hivyo, hatua hiyo nayo haijawa na msaada wowote katika kuupatia ufumbuzi mgogoro wa Yemen.
Kuna maswali mengi kuhusiana na utendaji wa Ismail Ould Sheikh mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Yemen na kwa mujibu wa fikra za waliowengi nchini humo ni kwamba, afisa huyo wa UN amekuwa na nafasi katika njama na katika kuifanya hali ya nchi hizo izidi kuwa mbaya. Hii ni kutokana na kuwa, misimamo yake imekuwa ikilenga zaidi katika kufunika hatua za ugombanishaji na uzushaji migogoro za Saudia. Mazingira yaliyowekwa na Saudia na waungaji mkono wake, nayo yameifanya mipango iliyopendekezwa na Ould Sheikh kutokuwa ya uwiano na kivitendo kuwa ni ya kupendelea upande mmoja. 
Mazingira haya yameifanya safari ya Ismail Ould Sheikh mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika Masuala ya Yemen huko Sana'a isipokelewe vizuri na wananchi pamoja na viongozi wa nchi hiyo.

RAIS ROUHANI AFANYA MAZUNGUMZO NA RAIS MPYA WA UFARANSA

Rais Hassan Rouhani wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema Tehran itaendelea kutekeleza makubaliano ya nyuklia ya Vienna.
Rais Rouhani aliyasema hayo jana jioni katika mazungumzo yake ya simu na Rais mpya wa Ufaransa, Emmanuel Macron na kusisitiza kuwa, Iran itatekeleza wajibu wake wa kimataifa kwa kutekelezwa ipasavyo makubaliano hayo yanayofahamika kama Mpango Kamili wa Pamoja wa Utekelezaji (JCPOA).
Aidha ameitaka Ufansa na Umoja wa Ulaya kwa ujumla kutekeleza barabara makubaliano hayo ya JCPOA. Kadhalika Dakta Rouhani amesisitizia umuhimu wa kuimarishwa uhusiano na ushirikiano wa kibiashara wa pande mbili kati ya Iran na Ufaransa katika  nyuga mbalimbali ikiwemo miundombinu na sekta ya uchukuzi.
Kwa upande wake, Macron amempongeza Rais Hassan Rouhani kwa kuchaguliwa tena kuongoza muhula wa pili, baada ya kushinda katika uchaguzi wa rais uliofanyika hivi karibuni hapa nchini.
Viongozi walioshiriki kusainiwa JCPOA mjini Vienna Julai 14, 2015
Kadhalika rais huyo mpya wa Ufanasa amesisitiza kuwa, JCPOA ni makubaliano muhimu ambayo yakitekelezwa ipasavyo na pande zote, yatatoa mchango mkubwa katika kuimarisha usalama wa eneo na kimataifa.
Aidha amesema Paris iko tayari kushirikiana na Tehran katika nyuga za uchumi, benki, utamaduni, utalii na elimu.
Ikumbukwe kuwa, tarehe 14 Julai 2015, Iran na nchi zinazounda kundi la 5+1 ambazo ni Uingereza, Ufaransa, Russia, China, Marekani na Ujerumani zilisaini mkataba kuhusiana na shughuli za nyuklia za Iran ambao utekelezaji wake ulianza Januari 16 mwaka uliopita wa 2016.