Friday, March 17, 2017

TRUMP ASEMA KOREA KAZKAZINI INAJIENDESHA VIBAYA SANA NA CHINA HAISAIDII

Rais wa Marekani Donald Trump ameilezea tabia ya Korea Kaskazini kuwa ni mbaya sana, na kuishtumu China kwa kutofanya vya kutosha kusaidia kubadili mwenendo wa taifa hilo ambalo ni mshirika wake wa karibu. Kauli ya Trump inakuja saa chache baada ya waziri wake wa mambo ya nje Rex Tillerson kusema hatua za kijeshi dhidi ya Korea Kaskazini ni jambo ambalo wanalizingatia baada ya kuonya kuwa sera ya uvumilivu wa kimkakati juu ya Korea Kaskazini imekwisha. Tillerson ambaye yuko ziarani Korea Kusini anatarajiwa kuizuru China hapo kesho na siku ya Jumapili atakutana na Rais wa China Xi Jinping.

No comments:

Post a Comment