Saturday, March 4, 2017

TRUMP AMSHUTUMU OBAMA KWA UDUKUZI

Rais wa Marekani Donald Trump amemshutumu mtangulizi wake Barack Obama kwa kutega simu za ofisi yake iliyoko New York wakati kampeini za urais. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Trump amesema kuwa ndio kwanza amegundua kuwa Obama alitega simu za ofisi yake iliyoko katika jengo la Trump Tower kabla ya ushindi wake lakini hakutaja chanzo cha taarifa zake hizo.Madai hayo ya Trump yanakuja huku utawala wake ukikabiliwa na maswali kuhusu wanachama wa kundi lake la kampeini kuwasiliana na Urusi kabla ya yeye kuapishwa kuwa Rais wa Marekani. Hotuba ya kwanza ya kiongozi huyo mpya wa Marekani bungeni wiki hii iligubikwa na ufichuzi kuwa mwanasheria mkuu Jeff Sessions alikutana mara mbili na balozi wa Urusi nchini Marekani mara mbili, jambo ambalo hakulifichua kabla ya kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu. Mashirika ya ujasusi ya Marekani yamesema ushawishi wa Urusi ulimsaidia Trump kushinda uchaguzi.

No comments:

Post a Comment