Friday, March 17, 2017

SHAMBULIO LA ANGA LA MAREKANI LAUA WATU 42 NA KUJERUHI 100 MSIKITINI SYRIA

Raia wasiopungua 42 wameuawa katika shambulio la anga la jeshi la Marekani lililolenga msikiti uliojaa waumini ndani yake karibu na mji wa Halab (Aleppo) kaskazini mwa Syria. Watu wengine zaidi ya 100 wamejeruhiwa katika shambulio hilo lililofanywa katika kijiji cha al-Jineh kilichopo kilomita 30 magharibi mwa mji wa Halab.
Kwa mujibu wa ripoti ya kanali ya televisheni ya Press TV shambulio hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo lilifanyika huku watu wapatao 300 wakiwa wamo ndani ya msikiti huo.
Abu Muhammad, ambaye ni mmoja wa wanakijiji amesema alisikio mlio mkubwa wa mripuko wakati msikiti huo ulipolengwa, mara baada ya sala ambapo kwa kawaida hufanyika darsa za wanaume msikitini humo.
Ndege za kivita za Marekani
Kwa mujibu wa ripoti, watu wengi walikuwa wangali wamekwama ndani ya msikiti huo ulioporomoka huku waokoaji wakijaribu kuwafukua na kuwatoa manusura kwenye vifusi.  
Katika taarifa yake, jeshi la Marekani limedai kuwa ndege za kivita za nchi hiyo ziliwalenga viongozi wa mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda. Hii ni katika hali ambayo kwa mujibu wa ripoti, jengo linalodaiwa kufanyika ndani yake kikao cha wanachama wa kundi hilo la kigaidi lipo umbali wa mita 15 tu kutoka msikiti ulioshambuliwa na ndege za Marekani.
Kamandi ya jeshi la Marekani aidha imetangaza kuwa itachunguza ripoti kwamba katika shambulio hilo ulilengwa msikiti na watu kadhaa wameuawa…

No comments:

Post a Comment