Friday, March 10, 2017

SERIKALI YA LEBANON: TUNAHITAJI SANA HIZBULLAH KWA AJILI YA ULINZI WA NCHI

Waziri Mshauri katika Masuala ya Ikulu ya Rais wa Lebanon, amesema kuwa nchi hiyo inaihitajia sana Harakati ya Hizbullah kwa ajili ya kukabiliana na kuzuia hujuma za utawala haramu wa Israel na makundi ya kigaidi dhidi ya ardhi ya nchi hiyo.
Sambamba na kusisitizia nafasi chanya ya harakati hiyo ya muqawama, Pierre Raffoul amesema kuwa, hata katika sherehe za kuapishwa Rais Michel Aoun alisema kuwa, silaha za Hizbullah si tu kwamba zinasaidia katika kusimamia usalama ndani ya nchi, bali hata nje ya mipaka ya Lebanon, zinahusika pia katika kuzuia chokochoko za Israel na makundi ya kigaidi. 
Pierre Raffoul, Waziri Mshauri katika Masuala ya Ikulu ya Rais wa Lebanon
Akifafanua kuwa silaha zinazotumiwa na Hizbullah ni silaha zinazotumiwa na jeshi la Lebanon, Raffoul amesema kuwa, ni silaha hizo hizo zilizoweza kuupigisha magoti utawala wa Kizayuni katika vita vya mwaka 2006. Itakumbukwa katika katika vita vya siku 33, mwaka 2006 kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel na Lebanon, Israel ilishindwa vibaya ambapo kutokana na kupata hasara kubwa, ililazimika kurudi nyuma na kusalimu amri. 
Wanamapambano shupavu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon, wanaoitia kiwewe Israel na Marekani
Hivi karibuni Rais Michel Aoun akihojiwa na televisheni ya CBC na gazeti la Misri la al-Ahram alisema kuwa, anaonga mkono kuendelea ushirikiano wa harakati ya Hizbullah na jeshi la Lebanon, udharura wa kulindwa silaha za harakati hiyo na uwepo wa Hizbullah nchini Syria katika vita dhidi ya makundi ya kigaidi na ukufurishaji ili kulinda taifa la Lebanon.
Aidha hivi karibuni Alexander Zasypkin, balozi wa Russia nchini Lebanon alisema kuwa, tangu awali harakati ya Hizbullah imekuwa na nafasi muhimu na chanya katika kupambana na magaidi nchini Syria na kudumisha usalama nchini Lebanon.

No comments:

Post a Comment