Friday, March 17, 2017

EU YATAKA UFANYIKE UCHAGUZI WA KIMATAIFA KUHUSU UNYAMA WALIOFANYIWA WAISLAMU WAROHINGYA

Umoja wa Ulaya (EU) umetaka Umoja wa Mataifa uanzishe uchunguzi kuhusu mateso, ubakaji na mauaji yaliyofanywa dhidi ya jamii ya wachache ya Waislamu Warohingya nchini Myanmar.
Rasimu ya azimio ambayo Umoja wa Ulaya umeiwasilisha kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa hapo jana la kuanzishwa uchunguzi wa kimataifa nchini Myanmar imetumia lugha kali zaidi kuliko rasimu inayofanana na hiyo iliyowasilishwa na EU hapo kabla.
Ripoti ya mwezi uliopita ya Umoja wa Mataifa iliyoandaliwa kulingana na ushahidi uliotolewa na manusura waliokuweko nchini Bangladesh inaonyesha kuwa jeshi na polisi ya Myanmar wametenda jinai dhidi ya Waislamu wa jamii ya wachache ya Rohingya kwa namna ya kuangamiza kizazi na jinai dhidi ya binadamu.
Waislamu Warohingya wanaoteseka nchini Myanmar
Aidha itakumbukwa kuwa ripoti iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch imeeleza kuwa kwa akali nusu ya wanawake na mabinti 101 wa Kiislamu wa jamii ya Rohingya waliohojiwa na Ofisi ya Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa walisema kuwa, walibakwa na kunajisiwa na askari wa serikali ya Myanmar.
Tarehe 23 na 24 za mwezi huu wa Machi, Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa linatazamiwa kuipigia kura rasimu ya azimio lililorejeshwa tena mbele ya baraza hilo kuhusu hali ya Waislamu wa Rohingya nchini Myanmar.
Umoja wa Mataifa umewataja Waislamu wa Myanmar kuwa jamii ya wachache inayokandamizwa zaidi dunaini..

No comments:

Post a Comment