Ambrose Mutinhiri, jenerali mstaafu wa jeshi
la Zimbabwe na mfuasi wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo Robert Mugabe
ameunda chama kipya cha siasa kinachojulikana kama Harakati Mpya ya
Kizalendo (NFP) kuchuana na rais Emmerson Mnangagwa katika uchaguzi mkuu
ujao.
Mutinhiri, ambaye ni veterani wa vita vya uhuru wa Zimbabwe
katika miaka ya 1970 alijitoa kwenye chama tawala cha ZANU-PF na
kujiuzulu kiti chake cha ubunge siku ya Ijumaa iliyopita na kukutana na
Mugabe siku ya Jumapili kumtaarifu juu ya kinachoendelea.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotoa hapo jana, NFP imetangaza kuwa chama
hicho kimeundwa na wananchama wa ZANU-PF na Wazimbabwe waliokasirishwa
na utaratibu usio wa kikatiba na wa udhalilishaji uliotumika kumuondoa
kihalifu uongozini rais Mugabe na wale kiliowataja kama wahalifu halisi
walioiharibu bila ya aibu demokrasia inayochipua ya Zimbabwe.
Hayo yanajiri katika hali ambayo duru za karibu na rais wa zamani wa
Zimbabwe zimeripoti kuwa Mugabe ana uchungu wa kuondolewa kwenye kiti
cha urais alichokalia kwa miaka 37 na kwamba ametangaza uungaji mkono
wake kwa chama kipya cha New Patriotic Front (NFP).
Mnamo mwezi Januari mwaka huu rais Emmerson Mnangagwa alitangaza
kuwa uchaguzi ujao wa Rais, Bunge na serikali za mitaa nchini Zimbabwe
utafanyika katika mazingira huru na ya haki.../
No comments:
Post a Comment