Mtoto mkubwa wa aliyekuwa rais wa Cuba, Fidel
Castro, Fidel Ángel Castro Díaz-Balart mwenye umri wa miakka 68 jana
alikutwa amejiua huko Havana, mji mkuu wa nchi hiyo.
Castro Díaz-Balart aliyefahamika kwa jina maarufu la “Fidelito” ametajwa na madaktari kwamba alikuwa ana matatizo ya msongo wa mawazo.
Kabla ya hapo Fidelito alikuwa mshauri wa kisayansi wa Baraza la
Serikali ya Cuba na alifanya kazi kama Makamu wa Rais wa Chuo Kikuu cha
Sayansi nchini Cuba, huku akiwa pia mwanafizikia wa nyuklia nchini humo.
Gazeti rasmi la Serikali ya Cuba la
Granma limeripoti kuwa; “Fidel Castro Diaz-Balart, alikuwa akipatiwa
matibabu na kundi la madaktari kwa miezi kadhaa kutokana na msongo wa
mawazo, ambao unatajwa kuwa chanzo cha yeye kujitoa uhai. Televisheni ya
taifa ya nchi hiyo imetangaza kwamba, mtoto huyo wa aliyekuwa rais wa
kwanza wa nchi hiyo alikuwa akipata matibabu katika miezi ya hivi
karibuni kama mgonjwa wa kutibiwa na kurudi nyumbani, baada ya kulazwa
hospitalini kwa muda. Baba yake, Mzee Fidel Castro, alifariki dunia
mwezi November 2016 akiwa na umri wa miaka 90 baada ya kuugua kwa muda
mrefu.
No comments:
Post a Comment