Mamilioni ya Wairan muda mchache kutokea hivi
sasa watamiminika mabarabarani kwa ajili ya kushiriki katika kilele cha
sherehe za miaka 39 ya ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu humu nchini.
Hii
ni katika hali ambayo maraajii wa kidini na viongozi mbalimbali wa
kisiasa wamewataka wananchi wa Iran kushiriki kwa umoja na kwa wingi
katika maandamano hayo ya mamilioni ya watu katika miji yote ya nchi
hii. Mjini Tehran maandamano hayo yatahudhuriwa na Rais Hassan Rouhani
ambaye kama kawaida atatoa hotuba katika uwanja wa Azad katikati mwa mji
wa Tehran, kama ambavyo pia watahudhuria viongozi wa ngazi mbalimbali
wa serikali.
Sherehe za ushindi wa Mapinduzi ya
Kiislamu nchini Iran huadhimishwa tarehe 22 Bahman kila mwaka sawa na
tarehe 11 Februari, ambazo hukumbushia siku muhimu ambayo Imam Ruhullah
Musawi Khomein alirejea kutoka uhamishoni na kisha kutangaza kuunda
serikali mpya inayoungwa mkono na wananchi tofauti na ile iliyokuwepo
wakati huo ambayo ilikuwa ni kibaraka wa Marekani, madola ya Magharibi
na utawala haramu wa Kizayuni wa Israel.
Hata hivyo suala la kufaa kuzingatiwa ni
kwamba, tangu Iran ilipojitangazia mfumo wa Kiislamu nchini hapa,
madola ya Magharibi yakiongozwa na Marekani na washirika wao wamekuwa
wakifanya njama za kila namna ikiwemo vikwazo vya kila upande kwa lengo
la kuipigisha magoti Iran ya Kiislamu, suala ambalo hata hivyo
limeendelea kugonga mwamba kwa kipindi chote cha tangu kupata ushindi
Mapinduzi ya Kiislamu na kuundwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
No comments:
Post a Comment