Viongozi wa upinzani katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo
wamewataka maafisa wa serikali kuchunguza ripoti ya shirika la habari la
Reuters iliyochapishwa wiki iliyopita, ikisema sehemu kubwa ya fedha
zinazolipwa na raia kwa ajili ya Pasipoti zinakwenda nje ya nchi. Ripoti
hiyo kuhusu mkata uliosainiwa mwaka 2015 baina ya serikali ya Kongo na
kampuni ya kibelgiji iitwayo Semlex kutengeneza paspoti za kisasa,
inaonyesha kuwa gharama ya paspoti moja ni dola 185 za kimarekani, na
kwamba nyingi kati ya fedha hizo huenda katika kampuni ya Semlex na
nyingine iliyosajiliwa katika Umoja wa Falme za Kiarabu ijulikanayo kama
LRPS. Aidha, ripoti hiyo inamnukuu mtu mwenye ujuzi kuhusu kampuni la
LRPS, akisema kampuni hiyo ni mali ya mtu mwenye uhusiano wa karibu na
Rais Joseph Kabila, aitwaye Makie Makolo Wagoi. Serikali ya Kongo na
Kampuni ya Semlex hawajatoa majibu yoyote kwa taarifa hizo.
No comments:
Post a Comment