Sunday, April 16, 2017

JARIBIO LA KOMBORA LA KOREA KASKAZINI LASHINDWA

Jaribio jipya la kufyatua kombora Korea kaskazini limeshindwa wakati liliporipuka baada ya kufyatuliwa Jumapili(16.04.2017) siku moja baada ya nchi hiyo kuonesha hazina yake ya makombora katika gwaride kubwa la kijeshi.
Nordkorea Fernsehübertragung der Militärparade in Pjöngjang (picture-alliance/AP Photo) Makombora ya Korea kaskazini katika maonesha ya gwaride
Kushindwa  huko , ambako  kunaonekana  kwa  umma  kama  kitu cha  fadhaa  kwa  serikali  ya  nchi  hiyo, kumekuja  huku  hali  ya wasi  wasi  ikiongezeka   katika  kanda  hiyo  kuhusiana  na  dhamira ya  Korea  kaskazini  kujipatia  silaha  za  kinyuklia.
"kombora  hilo  liliripuka  mara moja," wizara  ya  ulinzi  ya  Marekani ilisema  kuhusiana  na  jaribio  hilo  lililofanywa  mapema  leo asubuhi  ambalo taarifa  zake  zilipatikana  kupitia  jeshi  la  Korea kusini. Hata  hivyo  haikuwezekana  kufahamu  mara  moja ni  aina gani  ya  kombora  lilitumika  katika  jaribio  hilo, muda ambao unaonekana  kuwa  uliamuliwa  kwa  makusudi  kabisa.
Südkorea TV Nordkorea Propaganda (picture-alliance/AP Photo/A. Young-Joon) Kombora la Korea kaskazini likifyatuliwa
Jaribio  hilo  limekuwa  baada  ya  Korea  kaskazini  kuonesha karibu  makombora  60 , ikiwa  ni  pamoja  na  kile  kinachoshukiwa kuwa  kombora  jipya  linaloweza  kuvuka  mabara , katika  gwaride siku  ya  Jumamosi  kuadhimisha  miaka  105  ya  kuzaliwa  kwa muasisi  wa  taifa  hilo  Kim II-Sung.
Sherehe  hizo zilifanyika  mbele  ya  kamera za  mashirika  ya  habari duniani  yaliyoalikwa, ambayo  yalikuwapo  pia  Pyongyang wakati wa  jaribio  la  kurusha  kombora  hilo  lililoshindwa. Kushindwa  kwa kombora  hilo  kurushwa  kunakuja  masaa  machache  kabla  ya ziara  ya  Makamu  wa  Rais  wa  Marekani  Mike  Pence  nchini Korea  Kusini  ambako  mpango  wa  silaha  wa  taifa  hilo  lililoko upande  wa  kaskazini  utakuwa  ajenda  ya  juu.
Nordkorea Tanz in Pjöngjang (picture-alliance/dpa) Sherehe za kuadhimisha mwaka wa 105 wa kuzaliwa muasisi wa taifa la Korea kaskazini
Tabia  ya  ukaidi
Korea  Kaskazini  ina  tabia  ya  kurusha  makombora  kuadhimisha sherehe  muhimu  za  kisiasa, ama  kama  ishara  ya  ukaidi  mnamo wakati  maafisa  wa  ngazi  ya  juu  wa  Marekani  wanapofanya ziara  katika  eneo  hilo.
Waziri  wa  ulinzi  wa  Marekani  Jim Mattis  amesema  Trump amefahamishwa  kuhusu jaribio  hilo  la  hivi  karibuni  lakini "hakutoa maelezo  zaidi".
Großbritannien US-Verteidigungsminister Jim Mattis in London (Reuters/M. Dunham) Waziri wa ulinzi wa Marekani Jim Mattis
Tukio  la  leo Jumapili  la  kurushwa  kwa  kombora  kumefanyika majira  ya  alfajiri  kutoka  Sinpo , eneo  la  kurushia  makombora upande  wa  pwani  ya  mashariki  ya  Korea  kaskazini  ambako nchi  hiyo  ina eneo  la  kuegesha  meli.
Mwezi  Agosti mwaka  jana, kombora  lililorushwa  kutoka  katika nyambizi  kutoka  Sinpo liliruka  kilometa  500  kuelekea  Japan. Kiongozi  wa  Korea  kaskazini   Kim Jong-Un  amesifu  jaribio  hilo kuwa "ni  mafanikio  makubwa"  na  kusema  limeiweka  Marekani kuwa  karibu  na  mfumo  wa  kurusha  makombora  unaoweza kuhamishika.
Nordkorea Militärparade in Pjöngjang Kim Jong Un (picture-alliance/dpa/W. Maye-E) Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong-Un
Trump hajasema lolote
 Rais  Trump  amesema  mara  kadhaa atazuwia Pyongyang  kufikia lengo  lake  la  kutengeneza  makombora  yenye  silaha  za  nyuklia yanayoweza  kufika  nchini  Marekani.
Huku uvumi ukiongezeka  kuwa  Korea  kaskazini  inajitayarisha kufanya  jaribio  la  sita  la  makombora  ya  nyuklia  ametuma  meli ya  kivita  yenye  ndege  za  kivita  katika  rasi  ya  Korea--ishara  ya wazi baada  ya  Marekani  kufanya  shambulio  la  makombora  nchini Syria.
USA AIPAC-Treffen in Washington - Mike Pence (Reuters/J. Roberts) Makamu wa rais wa Marekani Mike Pence

No comments:

Post a Comment