Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Utafiti wa Utokomezaji Silaha (UNIDIR) imeonya kuwa mivutano inayoendelea kujiri duniani inaweza kusababisha maafa ya nyuklia.
Kwa mujibu wa tovuti ya gazeti la Daily Telegraph linalochapishwa London, Uingereza ripoti kamili iliyotolewa na Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Utokomezaji Silaha, inatoa taswira ya kuhuzunisha kuhusu kile kinachotarajiwa kuikumba dunia.Ripoti hiyo imeeleza kuwa kutotumiwa silaha za nyuklia tangu iliposhambuliwa kwa mabomu ya atomiki miji ya Hiroshima na Nagasaki hakumaanishi kuwa kuna uwezekano mdogo wa kutokea tena tukio kama hilo.
Kwa mujibu wa taasisi ya utafiti ya Umoja wa Mataifa japokuwa hakukutokea mripuko wa nyuklia wakati wa enzi za Vita Baridi lakini ripoti mbalimbali zilizopokewa kutoka nchi zenye kumiliki silaha za nyuklia zilikuwa zikionyesha kuwa ulitokea uripuaji mara kadhaa karibu na silaha hizo kufikia hadi ya kupigwa vingóra vya hali ya hatari.
Taasisi ya Umoja wa Mataifa ya Utafiti wa Utokomezaji Silaha (UNIDIR) imeonya kuwa kutokana na kuongezeka mifumo ya otomatiki ya uongozaji mitambo ya nyuklia hatari za kutokea miripuko ya silaha hizo imeongezeka.../
No comments:
Post a Comment