Mechi hiyo ya ligi ya mabingwa barani Ulaya, Champions
League, kati ya Borussia Dortmund na Monaco, ilikuwa ichezwe jana
(11.04.2017) katika uwanja wa Signal Iduna Park mjini Dortmund.
Basi la timu ya Borussia Dortmund limeharibiwa na abiria mmoja
kujeruhiwa baada ya milipuko mitatu kutokea karibu na basi hilo
lililokuwa njiani kuelekea uwanja wa Signal Iduna Park umbali wa kiasi
kilometa kumi ambako mechi ya ligi ya mabingwa, Chamiopns League,
ilitarajiwa kuchezwa. Tukio hilo limetokea mwendo wa saa moja usiku saa
za Ujerumani.
Msemaji wa jeshi la polisi katika jimbo la North Rhine Westphalia, Gunnar Wortmann, aliliambia shirika la habari la Associated Press, "Basi lilianza safari kutoka hoteli ya timu ya Dortmund wakati milipuko mitatu ilipotokea. Milipuko mitatu ilitokea karibu na basi hilo lilipokuwa njiani kuelekea uwanjani na kwamba mchezaji mmoja amejeruhiwa na dirisha moja kuharibiwa."
Beki wa Dortmund ajeruhiwa
Gazeti la Ujerumani la Bild limeripoti kwamba beki wa Borussia Doetmund Marc Bartra amejeruhiwa na kupelekwa hospitali. Klabu ya Dortmund imetuma taarifa katika mtandao wa kijamii wa Twitter ikisema mchezaji huyo yuko salama na hakuna kitisho chochote ndani na nje ya uwanja wa Signal Iduna Park.
Mkurugenzi wa klabu ya Dortmund, Hans-Joachim Watzke, alithibitisha kujeruhiwa kwa Bartra, akisema ameumia mkononi na kuwa majeruhi si hatari kwa maisha yake.
Msemaji wa polisi ya Dortmund, Nina Vogt, alisema wachunguzi bado hawafahamu chanzo cha milipuko iliyotokea wakati timu ya Borussia Dortmund ilipokuwa ikijiandaa kuondoka hotelini kuelekea uwanjani kuchuana na Monaco. Polisi imesema inalichukulia tukio hilo kuwa shambulizi. Hata hivyo hakuna dalili kuonyesha ni shambulizi la kigaidi.

Basi la Borussia Dortmund likionekana hapa baada ya mlipuko karibu na hoteli ya timu hiyo kabla mechi
Dortmund
iliamua kuiahirisha mechi hiyo ya duru ya kwanza ya robo fainali ya
ligi ya mabingwa barani Ulaya na kuutangaza uamuzi huo kupitia ukurasa
wake wa Twitter ikiongeza kuwa tiketi zote za mashabiki waliotaka
kuutazama mtanange huo zinabaki kuwa halali na zitatumika leo.
No comments:
Post a Comment