Tuesday, June 12, 2018

TRUMP NA KIM WATIA SAINI MAKUBALIANO YA KIHISTORIA

Rais wa Marekani Donald Trump na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un wamekubaliana kuondoa kabisa silaha za kinyuklia katika  rasi ya Korea katika makubaliano ya  pamoja  ya kihistoria.

     Singapore Summit Donald Trump Kim Jong Un Unterzeichnung (Reuters/J. Ernst)
Viongozi  hao  walikamilisha siku ya kihistoria ambayo ilishuhudia viongozi hao wawili wakikutana kwa  mara  ya  kwanza kabisa.
Katika  mkutano  huo Trump  ameahidi  kuipatia  Korea  kaskazini  uhakikisho  wa  usalama wake  pamoja  na  kutangaza  katika  mkutano  na  waandishi  habari baadaye  kwamba  Marekani  na  Korea  kusini  zitaacha  luteka  ya pamoja  ya  kijeshi kama Korea kaskazini  inavyodai.
Singapur Gipfel Kim Jong Un Donald Trump (Reuters/A. Wallace)
Kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un (kushoto) na rais wa Marekani Donald Trump wakipeana mikoni
Katika  waraka  wenye vipengee  vinne, Marekani  na  Korea kaskazini  zimeazimia  kuweka  uhusiano  mpya  kati  ya  nchi  hizo mbili, kujenga   utawala  imara  na  endelevu  kuelekea  amani akisisitiza  azimio  la  Panmunjeom  kutoka  Aprili  27.
Katika  mkutano  na  waandishi  habari leo rais  Donald Trump  wa Marekani  amesema  kwamba  jeshi  la  Marekani  litaacha  kufanya mazowezi  ya  pamoja  na  Korea  kusini  yakiilenga  Korea kaskazini, akisema  yanaongeza  hali  ya  wasi  wasi na  kuyasitisha kutasaidia  kuhifadhi  fedha  nyingi  zinazotumika  katika  mazowezi hayo. Pia  amesema  atamwalika  kiongozi  wa  Korea  kaskazini katika  ikulu  ya  marekani White house na  kwamba   binafsi angependa  kutembelea  mji mkuu  wa  Korea  kaskazini  Pyongyang.
Nchi  hizo  mbili  hufanya  mazowezi  ya  kijeshi  kila  mwaka  ambayo yanaikera  Korea  kaskazini , ambayo  imekuwa  kwa  muda  mrefu ikidai kusitishwa  kwa  mazowezi  hayo na  mara  nyingi  hujibu  kwa kuchukua  hatua  zake, na  kusababisha  kuongezeka  kwa  hali  ya wasi  wasi. 
Singapur - Präsident Donald Trump gemeinsam Unterschriebenes Dokument nach Treffen mit Kim Jong Un (Reuters/J. Ernst)
Rais Trump akionesha waraka uliotiwa saini baina yake na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un
Kim amshukuru  Trump
Wakati  wa  kutia  saini  makubaliano  hayo  kati  ya Trump  na  Kim leo  asubuhi, rais  Trump  alisema  pande  zote  mbili zimefurahi  kutia  saini  makubaliano  hayo.
"Tunatia  saini  waraka  muhimu  sana, waraka  ambao una maelezo mapana. na  tutajadili  hili  kwa  kina. Kwa  hivi  sasa naamini  mtapata nakala kwa  niaba  ya  mwenyekiti Kim  na mimi. Na wote tunafahari  kubwa  kutia  saini  waraka  huu. Asante."
Kwa  upande  wake  kiongozi  wa  Korea  kaskazini  Kim Jong Un alimshukuru  rais  Trump  kwa  kukubali  kufanyika  mkutano  huo.
"Leo tulikuwa  na  mkutano  wa  kihistoria  na  kuamua  kuacha nyuma  yaliyopita. Na  tuko  tayari  kutia  saini  waraka  huu  wa kihistoria. Dunia  itaona  mabadiliko  makubwa. Napenda kueleza  shukurani  zangu  kwa  rais Trump  kwa  kufanikisha mkutano  huu. Asante.
Kuhusu  vikwazo  dhidi  ya  Korea  kaskazini  rais  Trump  amesema kwa  hivi  sasa  vikwazo  hivyo  vitaendelea , lakini  anaangalia uwezekano  wa  kuviondoa.
Donald Trump Pressekonferenz Singapur (Reuters/J. Ernst)
Rais Trump akiwa katika mkutano na waandishi habari baada ya kutia saini makubaliano na kiongozi wa Korea kaskazini Kim Jong Un
Rais  wa  Marekani  amesema  pia  kwamba  kiongozi  wa  Korea kaskazini  Kim Jong Un ana  nia  thabiti  ya  kuharibu  kabisa maeneo  ambayo  nchi  hiyo  inafanyia  majaribio  silaha  zake.
Kwa  upande  mwingine waziri  mkuu  wa  Japan  Shinzo  Abe  na mwenzake  wa  Malaysia  mahathir Mohammed wamekubaliana  leo kufanyakazi  kwa  pamoja  kupambana  na  mipango  ya  kinyuklia  na makombora  ya  Korea  kaskazini. Viongozi  hao  wamesema wanataka  kutuma  ujumbe  mkali  kwa  Korea  kaskazini  kuhusu suala  hilo.  Waliysema  hayo  katika  mkutano  na  waandishi  habari kufuatia  mkutano  wao  mjini  Tokyo

No comments:

Post a Comment