Tuesday, May 23, 2017

19 WAUAWA KATIKA HUJUMA YA KIGAIDI MANCHESTER, UINGEREZA

Mlipuko huo ulitokea baada ya tamasha la muziki katika ukumbi wa Manchester Arena Jumatatu (22.05.2017) usiku. Mlipuko ulitokea wakati watu walipokuwa wakiondoka baada ya tamasha kukamilika.

Großbritannien Anschlag in Manchester (Getty Images/D. Thompson)
Polisi nchini Uingereza wanasema watu wasiopungua 22 wameuawa na wengine 59 kujeruhiwa kwenye mlipuko uliotokea mwishoni mwa tamasha la muziki la mwanamuziki wa Marekani Ariana Grande mjini Manchester kaskazini magharibi mwa England. Watoto ni miongoni mwa waliouawa katika shambulizi hilo la kigaidi linaloulizwa kuwa baya kabisa katika kipindi cha miaka 12. Maafisa wawili wa Marekani wamesema mshambuliaji wa kujitoa muhanga anashukiwa kuhusika na mlipuko huo.
Mashabiki waliokuwa wakipiga mayowe, wengi wao vijana wanarika, walikimbia kutoka eneo la tukio wakiwa na hofu baada ya mlipuko huo wa bomu baada ya tamasha kukamilika."Nilihisi moto katik shingo yangu na nilipotazama nikaona maiti kila mahala," alisema Elena Semino, aliyekuwa akimtafuta mtoto wake wa kike wa umri wa miaka 17, alipozungumza na gazeti la Guardian.
Semino, ambaye mwenyewe alijeruhiwa, alisema alikuwa amesimama kando ya ofisi ya kutoa tiketi ya ukumbi wa Manchester Arena wenye nafasi za watu 21,000 wakati mlipuko ulipotokea.
Großbritannien Polizeieinsatz in Manchester (picture-alliance/ZUMA/London News Pictures/J. Goodman)
"Mlipuko mkubwa kama wa bomu ulitokea ambao ulimfanya kila mtu kujawa na taharuki na sote tulikuwa tunajaribu kukimbia kutoka ukumbini," alisema Majid Khan, mwenye umri wa miaka 22 ambaye alikuwa katika tamasha hilo na dada yake.
Magari ya kubebea wagonjwa na timu za wataalamu wa kutengua mabomu walikimbi katika eneo hilo huku jamaa wa familia wakiwatafuta wapendwa wao na wakazi wakifungua milango ya nyumba zao kuwakaribisha watu waliokuwa wamehudhuria tamasha hilo baada ya safari za treni kufutwa.
"Watoto ni miongoni mwa watu 22 waliouliwa katika shambulizi hilo, huku watu 59 wakijeruhiwa," alisema Ian Hopkins, Mkuu wa jeshi la polisi Geater Manchester, mapema siku ya Jumanne. 
Kampeni za siasa zasitishwa
Waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May amelaani vikali shambulizi hilo la kinyama na kusitisha kamepni yake kuelekea uchaguzi mkuu Juni 8 kama alivyofanya kiongozi mkuu wa upinzani, Jeremy Corbyn. "Tunawakumbuka wahanga na kuziombea dua familia za wote walioathiriwa," alisema Bi May, ambaye anatarajiwa kuongoza kikao cha dharura cha kamati ya usalama kuanzia saa tatu asubuhi.
"Tunafanya juhudi kupata taarifa kamili kuhusu kile kinachochukuliwa na polisi kuwa shambulizi la kigaidi," alisema May katika taarifa. 
Rais wa China Xi Jinping alituma risala zake za rambirambi kwa Malkia Elizabeht wa Uingereza kuhusu mlipuko wa mjini Manchester.
Polisi wa Manchester wanasema wanashirikiana na polisi ya taifa na mashirika ya kijasusi kuchunguza mlipuko huo. Meya wa mji wa London Sadiq Khan ametuma risala zake za rambirambi kwa jamii za wahanga na amesema mji wa London unasimama pamoja na mji wa Manchester kufuatilia tukio hilo.

WATU MILIONI 31 WALILAZIMIKA KUWA WAKIMBIZI NCHINI MWAO 2016

Umoja wa Mataifa umesema watu zaidi ya milioni 31 walilazimika kuwa wakimbizi ndani ya nchi zao mwaka uliopita wa 2016 lote duniani.
Ripoti ya UN imesema kuwa, idadi kubwa ya wakimbizi hao wa ndani ya nchi ilisajiliwa huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Syria, kutokana na kushadidi migogoro na majanga ya kimaumbile.
Jan Egeland, Mkuu wa Baraza la Wakimbizi la Norway amesema mwaka uliopita, kwa kila sekunde, mtu mmoja alilazimika kuhama makazi yake kutokana na migogoro, mapigano na majanga ya kimaumbile kama mafuriko, maporomoko ya ardhi na mikasa ya moto.
Kambi za wakimbizi Kongo DR
Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema kuwa, watu 922,000 walifurushwa makwao mwaka jana 2016 huko Kongo DR, 824,000 nchini Syria, Wairaqi 659,000, Waafghani 653,000 huku watu 501,000 wakilazimika kuwa wakimbizi wa ndani nchini Nigeria.
Mwezi uliopita, Yvon Edoumou, afisa katika Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Masuala ya Kibinadamu (OCHA) alisema kuwa, ofisi hiyo imesajili wakimbizi wa ndani milioni 1.09 katika mkoa wa Kasai, katikati mwa Kongo kuanzia Aprili Mosi mwaka huu.

SAUDIA MNUNUZI MKUBWA ZAIDI WA SILAHA ZA MAREKANI, ISRAEL MPOKEZI MKUBWA ZAIDI WA MISAADA YA KIJESHI YA MAREKANI

Utawala wa Kizayuni wa Israel umebainisha wasiwasi wake kuhusu Marekani kuiuzia Saudi Arabia silaha zenye kugharimu mabilioni ya dola katika hali ambayo Israel yenyewe inapokea misaada ya silaha za kisasa zaidi kutoka Marekani.
Yuval Steinitz Waziri wa Nishati wa Israel Jumapili alibainisha wasiwasi wake kuhusu mkataba wa Marekani kuiuzia Saudia silaha zenye thamani ya mabilioni na dola na kudai kuwa mkataba huo uteiletea Israel matatizo. 
Jumamosi Mei 20 Rais Donald Trump wa Marekani aliwasili Saudia na hadi Mei 22 alipoondoka Riyadh na kuelekea Tel Aviv kukutana na wakuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel. Moja ya matukio muhimu zaidi ya safari ya Trump mjini Riyadh ni kutiwa saini mkataba wa ununuzi silaha zenye thamani ya dola bilioni 350 na hilo ndilo lililomtia wasi wasi waziri wa nishati wa utawala wa Israel. Lakini je, ni kweli kuwa mkataba huo wa silaha utakuwa na taathira hasi kwa Israel hadi kufikia kiwango cha waziri huyo au wengine kuwa na wasi wasi kiasi hicho?
Uhusiano wa Israel na Saudia katika miaka ya hivi karibuni umetoka katika kiwango cha 'uhasama' na kuwa wa 'mashindano'. Kwa hivyo hata kama mikataba ya kijeshi ya Marekani na Saudia inaitia Israel wasiwasi si kwa kiwango cha kutisha. Aidha uhusiano wa karibu wa Israel na Saudi Arabia umezidi kudhihirika katika miaka ya hivi karibuni baada ya maafisa wa tawala hizo mbili kukutana maeneo mbali mbali.
Trump na Salman wakitia saini mapatano ya kuiuzia Saudia silaha
Nukta nyingine ni kuwa ingawa Israel na Saudia ni waitifaki wakubwa zaidi wa Marekani Asia Magharibi (Mashariki ya Kati) lakini ukweli ni kuwa Israel inapewa uzito na umuhimu mkubwa zaidi na Marekani kuliko Saudia. Ni kwa msingi huo ndio maana Marekani haiwezi kuchukua hatua yoyote yenye kutia hatarani usalama wa utawala haramu wa Israel.
Maudhui nyingine hapa ni kuwa, pamoja na kuwa Marekani imeafiki kuiuzuia Saudi Arabia silaha zinazogharimu mabilioni ya dola lakini katika upande wa pili inaipatia Israel silaha za kisasa kabisa ambazo katu haiwezi kuiuzia Saudia.
Kwa hivyo katika hali ambayo Marekani inachangia kueneza hofu na chuki dhidi ya Iran na kwa msingi huo kuibua adui bandia ili kuishawishi Saudia na madola mengine ya Kiarabu yanunue silaha za Kimarekani lakini kile ambacho ni muhimu kwa Marekani ni uhusiano wake na Israel ambao umejengeka katika msingi wa  'kufungamana na kulinda usalama' wa utawala huo.
Nukta ya nne hapa ni kuwa makubaliano ya Marekani kuizuia Saudia silaha kimsingi ni kwa faida ya Marekani. Kama alivyotamka Trump baada ya kutiwa saini mapatano hayo, Marekani imeweza kuvutia uwekezaji wa Saudia na hilo litapelekea Wamarekani kupata ajira. Kimsingi ni kuwa Marekani inapora utajiri wa mafuta wa Saudia kwa kuipatia silaha duni na kwa bei ya juu huku ikiipatia Israel msaada wa silaha za kisasa kabisa.
Ikumbukwe kuwa Septemba mwaka 2016, Marekani na Israel zilitiliana saini mapatano makubwa zaidi ya kijeshi. Kwa mujibu wa mapatano hayo, Marekani iliahidi kuwa, katika kipindi cha miaka 10 ijayo, itaipatia Israel msaada wa kijeshi wenye thamani ya dola bilioni 38.
Ndege za kivita aina ya F18 zilizotengenezwa Marekani
Ukweli ni kuwa mkataba wa kijeshi wa Marekani na Saudia hautakuwa na athari yoyote mbaya kwa Israel na hatua ya waziri wa nishati wa Israel kudai kuwa eti ana wasi wasi ni kwa ajili tu ya kuishinikiza Marekani iupe utawala huo misaada zaidi.
Mkataba wa kijeshi wa Marekani na Saudia una malengo na manufaa ya  kiuchumi zaidi kuliko ya kijeshi kama ambavyo pia utawala wa Kizayuni wa Israel umetia saini mkataba wa kuiuzia India mfumo wa kujihami angani wenye thamani ya dola milioni 630. India pia imetiliana saini mapatano mengine ya miaka 10 na shirika moja la kijheshi la Israel.

Monday, May 22, 2017

MWANAMKE WA UJERUMJANI AUWAWA KABUL

Mwanamke mwananchi wa Ujerumani ameuwawa mjini Kabul ambapo repoti za awali zimedokeza kwamba mauaji hayo yametokea katika mji huo mkuu wa Afghanistan wakati wa jaribio la utekaji nyara.
Kabul Afghanistan Polizei (picture alliance/AP Photo/M.Hossaini)
Wizara ya mambo ya nje wa Ujerumani imethibitisha kwamba mwanamke wa Ujerumani ameuwawa wakati wa usiku katika mji mkuu huo mkuu wa Afghanistan lakini ufafanuzi zaidi kuhusu mauaji hayo haukuweza kufamika mara moja.Mwanamke huyo hakutajwa jina wala hayakutolewa malezo ya jinsi alivyouwawa.
Najib Danish naibu msemaji wa wizara ya mambo ya ndani amesema mwanamke mmoja wa Ujerumani na mlinzi wa usalama wa Afghanistan wameuwawa wakati mwanamke mmoja wa Finland alitekwa nyara kutoka nyumba moja ya kulala wageni mjini Kabul wakati wa saa tano na nusu usiku.
Karolina Romanoff msemaji kutoka wizara ya mambo ya nje ya Finland amethibitisha kwamba raia mmoja wa Finland ametekwa nyara lakini hana ufafanuzi zaidil.Wizara ya mambo ya nje imesema katika taarifa inataka kuachiliwa huru mara moja kwa mtu huyo aliyetekwa nyara.
Scott Brestlin mfanyakazi wa kampuni yenye makao yake nchini Sweden ya Opereration Mercy ameliambia shirika la habari la Sweden TT kwamba mmojawapo wa wafanyakazi wake hajulikani alipo na wameitisha mkutano wa dharura.
Wajerumani waonywa kutokwenda Afghanistan
Afghanistan Kabul Tatort Entführung Deutsche getötet (Reuters/O.Sobhani) Mvulana akiendesha baiskeli mbele ya nyumba alikouwawa mwanamke wa Ujerumani na mlinzi wa Afghanistan.
Wizara ya mambo ya nje ya Ujerumani imekuwa ikiwaonya watu kwa muda mrefu kutosafiri kwenda Afghanistan wakati huo huo serikali ya Ujerumani imekuwa ikishinikiza kuorodheshwa kwa taifa hilo kama taifa salama ili kuwezesha kurudishwa kwa wakimbizi ambao maombi yao ya kuomba hifadhi yamekataliwa.
Hakukuwa na taarifa ya mara moja kudai kuhusika aidha na shambulio hilo au utekaji nyara.Utekaji nyara umekuja kuwa tatizo kubwa nchini Afghanistan na kwa kawaida huwaathiri wananchi wa Aghanistan ambao hutekwa nyara kwa ajili ya kudaiwa kulipa fedha za kuwagombolea.Hata hiyo wageni mara nyingine wamekuwa wakitekwa nyara nchini humo ili kuzishinkiza serikali zao.
Kabul imekumbwa na makundi ya uhalifu yalioandaliwa ambayo hupanga utekaji nyara kwa nia ya kujipatia fedha za ugombozi kwa kuwalenga mara nyingi wageni na raia matajiri wa nchi hiyo na mara nyengine kuwakabidhi makundi ya waasi.
Hali inazidi kuwa mbaya
TEST TEST TEST (AFP/Getty Images) Polisi wa Afghanistan wakidumisha usalama Kabul.
Matumizi ya nguvu yaonyesha hali kuzidi kuwa mbaya nchini Afghanistan ambayo inakabiliana na uasi wa kundi la Taliban na makundi mengine.
Taliban imedai kuhusika na mashambulizi yaliyoratibiwa katika kitongoji cha Shah Joy ilioko katika jimbo la Zabul ambalo ni pigo jengine kwa Jumuiya ya Kujihami ya NATO ikisaidiwa na vikosi vya Afghanistan.
Asubuhi ya Jumapili (21.05.2017) kundi la wapiganaji wa Taliban wakiwa na silaha nzito na nyepesi walifanya mashambulizi hayo ya kuratibiwa kwa vituo kadhaa vya ukaguzi wa polisi na kuuwa polisi 20.
Gavana wa jimbo hilo Bismillah Afghamal ameliambia shirika la habari la AFP kwamba polisi wengine takriban 15 wamejeruhiwa katika mapigano hayo. Shambulio hilo la karibuni kabisa miongoni mwa mashambulizi ya Taliban linaonyesha kuongezeka kwa nguu za uasi zaidi ya miaka 15 tokea walipotimuliwa madarakani na uvamizi wa Marekani hapo mwaka 2001.

RAMAPHOSA ATAHADHARISHA AFRIKA KUSINI KUGEUKA NCHI YA KIMAFIA

Makamu wa Rais wa Afrika Kusini ametahadharisha juu ya nchi hiyo kugeuka na kuwa ya Kimafia.
Cyril Ramaphosa Makamu wa Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini sambamba na kumkosoa Zuma amesisitiza kuwa, kama chama tawala wa ANC kinataka kisipoteze himaya na udhibiti wa jamii ya nchi hiyo, basi hakipaswi kuruhusu Afrika Kusini igeuke na kuwa nchi ya Kimafia.
Makamu huyo wa Rais wa Afrika Kusini anayetajwa kama mrithi wa Rais Zuma katika uchaguzi ujao, ametoa wito wa kuweko uchunguzi huru kuhusiana na faili la ufisadi ambalo limewatia katika alama ya swali baadhi ya viongozi wa ngazi za juu wa nchi hiyo.
Maandamano dhidi ya  Rais Zuma yamekuwa yakifanyika mara kwa mara nchini Afrika Kusini
Chama tawala nchini Afrika Kusini katika miaka ya hivi karibuni kimepungua umaarufu wake kutokana na viongozi wa ngazi za juu wa chama hicho akiwemo Rais Jacob Zuma kukabiliwa na tuhuma mbalimbali zikiwemo za ufisadi na utovu wa maadili.
Disemba mwaka huu chama hicho kinatarajiwa kumtangaza mrithi wa Rais Jacob Zuma anayemaliza muda wake ambapo Cyril Ramaphosa, Makamu wa Rais wa nchi hiyo amekuwa akitajwa kama chaguo la chama hicho katika uchaguzi ujao uliopangwa kufanyika nchini humo mwaka 2019.

KUENDELEA SIASA ZA KUPENDA VITA ZA MAREKANI KATIKA PENINSULA YA KOREA

Katika hali ambayo baadhi ya duru za habari zimearifu kupungua misimamo ya pande mbili kuhusiana na mgogoro wa Peninsula ya Korea, yaani Marekani na Korea Kaskazini, Washington imetuma meli yake ya kivita aina ya USS Ronald Reagan katika maji ya karibu na Korea Kaskazini.
Kabla ya hapo pia Marekani ilituma meli ya USS Carl Vinson kwenda katika maji ya Peninsula ya Korea suala ambalo lilisababisha kuongezeka mvutano katika eneo hilo. Korea Kaskazini iliitaja hatua ya kutumwa meli hiyo katika maji ya eneo hilo kuwa ni sawa na kutangaza vita huku ikiionya vikali Washington kutokana na madhara makubwa yanayoweza kutokea kufuatia hatua hiyo ya kichokozi. Mbali na Pyongyang, Uchina pia ilikutaja kupenda vita kwa Washington katika eneo hilo kuwa kunatokana na siasa za kiuhasama za baharini ambapo ilimtaka Rais Donald Trump wa Marekani kuachana na mwenendo huo.
Kiongozi wa Korea Kaskazini akikagua marubani wa kike
Kwa kuzingatia indhari za mara kwa mara za Korea Kaskazini juu ya utumwaji wa meli zaidi ya vita katika maji yake, hivyo kitendo hicho cha Washington si cha kustaajabisha sana. Kuhusiana na suala hilo kuna nukta kadhaa za kufaa kuashiriwa. Kwanza ni kuwa, kutumwa meli zaidi za kivita za Marekani katika eneo kunabainisha nafasi athirifu za kimtazamo na siasa za majenerali wa jeshi la nchi hiyo kwa nafasi yao ya kimaamuzi katika ikulu ya nchi hiyo White House. Hata hivyo suala hilo halihusiani tu na eneo pekee la Peninsula ya Korea na mashariki mwa Asia, bali linashuhudiwa pia nchini Afghanistan, Syria, Iraq na Yemen, ambapo makamanda wa jeshi la Marekani wanahusika na kupanga ratiba za kuongeza majeshi ya nchi hiyo ndani ya mataifa hayo.
Meli ya kivita ya Marekani iliyoamuriwa kwenda katika maji ya karibu ka Korea Kaskazini
Amma nukta ya pili ni kwamba, baadhi ya wachambuzi wa mambo wameitaja hatua ya Marekani ya kutuma meli ya USS Ronald Reagan katika maji ya Peninsula ya Korea kuwa yenye shabaha ya mwisho ya Washington kwa ajili ya kuandaa mazingira ya kufanya mazungumzo na Pyongyang. Hii ni kusema kuwa hadi hivi sasa Pyongyang na Washington zimejiandaa kufanya mazungumzo kwa masharti maalumu, hivyo kitendo cha Marekani cha kuendelea kutuma zaidi meli zake za kivita katika maji hayo ni aina fulani ya kuandaa mazingira kwa ajili ya kuisukuma Korea Kaskazini kwenye meza ya mazungumzo. Pamoja na hayo inaonekana kwamba, Moon Jae-in rais mpya wa Korea Kusini haoni kitendo cha kutunishiana misuli baina ya Korea Kaskazini na Marekani kama kinaweza kuandaa mazingira ya kufanyika mazungumzo ya pande mbili. Na ni kwa ajili hiyo ndio maana akautaka Umoja wa Mataifa kwa kushirikiana na Seoul, usaidie katika utatuzi wa mgogoro wa eneo la Peninsula ya Korea.
Moon Jae-in, Rais Mpya wa Korea Kusini
Katika mazungumzo ya simu na António Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini, sambamba na kusisitizia suala hilo, alisema kuwa, kuhitimishwa mgogoro wa eneo la Peninsula ya Korea kunahitajia ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na serikali ya Korea Kusini. Suala hilo linaonyesha kwamba, serikali Seoul ambayo inahesabika kuwa muitifaki mkubwa wa Washington, haikubaliani na siasa za Marekani kuhusiana na eneo hilo kama ambavyo inazitambua siasa hizo kuwa ndizo zinazochafua usalama wa eneo hilo. Marekani pia inafahamu vyema kwamba, mgogoro wa Peninsula ya Korea ikiwa hautatatuliwa kwa njia za kisiasa na badala yake zikatumika njia za kijeshi, basi utasababisha maafa makubwa. Hata kama kwa upande wa usalama, Marekani inaonekana iko mbali na Peninsula ya Korea, lakini kambi zake za kijeshi zilizoko Korea Kusini na Japan zitakuwa za kwanza kuangamizwa na makombora ya Korea Kaskazini. Ni kwa ajili hiyo ndio maana makamanda wa jeshi la Marekani hawapendelei kumaliza mgogoro wa eneo hilo kwa njia za kijeshi.
Kim In Ryong, Naibu Balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa
Pamoja na hivyo, makamanda wa nchi hiyo wanadai kuwa, kuongezeka mvutano wa eneo hilo kumeilazimisha Washington kutuma zana za baharini katika maji ya eneo zikiwemo meli za kivita kwa shabaha ya kufanya doria. Suala hilo lina maana kwamba, Marekani inatumia mgogoro huo kwa ajili ya kuimarisha uwepo wake katika eneo hilo kwa nia ya kuzidi kuizingira China. Wakati huo huo, naibu balozi wa Korea Kaskazini katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, sasa umefika wakati Marekani kuachana na siasa zake za uhasama dhidi ya Pyongyang. Kim In Ryong amesema kuwa, kabla ya Marekani kuanza mazungumzo yoyote na Korea Kaskazini, kwanza inatakiwa kuachana na siasa zake za uadui dhidi ya nchi yake.

Sunday, May 21, 2017

EU YAKATAA OMBI LA MUSEVENI NA MAGUFULI LA KUIONDOLEA VIKWAZO BURUNDI

Balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania amekataa ombi la marais wa Tanzania na Uganda la kuutaka umoja huo uifutie vikwazo Burundi.
Roeland van de Geer amenukuliwa na mtandao wa habari wa Africa Times akitoa msimamo huo wa Umoja wa Ulaya baada ya marais wa Tanzania na Uganda kutaka kuondolewa vikwazo Burundi na kusema kuwa vikwazo hivyo vitaendelea hadi hali ya kisiasa itakapobadilika nchini humo.
Ikumbukwe kuwa katika mkutano wa kukabidhiana uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC uliofanyika jijini Dar es Salaam Tanzania siku ya Jumamosi, Rais Yoweri Museveni wa Uganda na mwenzake wa Tanzania, John Pombe Magufuli waliutaka Umoja wa Ulaya ufute vikwazo ulivyoiwekea Burundi.

Roeland van de Geer, balozi wa Umoja wa Ulaya nchini Tanzania
Mwenyekiti mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Rais Yoweri Museveni wa Uganda alisema kuwa, jumuiya hiyo inapinga uamuzi wa Umoja wa Ulaya wa kumuwekea vikwazo mwanachama wa jumuiya hiyo.
Mgogoro mkubwa wa kisiasa umeikumbwa Burundi tangu Rais Pierre Nkurunziza wa nchi hiyo alipoamua kugombea tena urais kwa mara ya tatu mfululizo huku wapinzani wakisema kuwa huo ulikuwa ni ukiukaji wa wazi wa makubaliano ya Arusha, Tanzania, yaliyomaliza vita vya ndani nchini Burundi.
Uchaguzi mkuu wa Burundi ulisusiwa na wapinzani, na Umoja wa Ulaya nao ukaiwekea vikwazo nchi hiyo. Mgogoro huo umesababisha matatizo mengi yakiwemo mauaji na wimbi kubwa la wakimbizi wa ndani na nje ya Burundi.

Rais Pierre Nkurunziza wa Burundi