Rais wa Marekani Donald Trump amemshutumu mtangulizi wake Barack
Obama kwa kutega simu za ofisi yake iliyoko New York wakati kampeini za
urais. Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Trump amesema kuwa ndio kwanza
amegundua kuwa Obama alitega simu za ofisi yake iliyoko katika jengo la
Trump Tower kabla ya ushindi wake lakini hakutaja chanzo cha taarifa
zake hizo.Madai hayo ya Trump yanakuja huku utawala wake ukikabiliwa na
maswali kuhusu wanachama wa kundi lake la kampeini kuwasiliana na Urusi
kabla ya yeye kuapishwa kuwa Rais wa Marekani. Hotuba ya kwanza ya
kiongozi huyo mpya wa Marekani bungeni wiki hii iligubikwa na ufichuzi
kuwa mwanasheria mkuu Jeff Sessions alikutana mara mbili na balozi wa
Urusi nchini Marekani mara mbili, jambo ambalo hakulifichua kabla ya
kuteuliwa kuwa mwanasheria mkuu. Mashirika ya ujasusi ya Marekani
yamesema ushawishi wa Urusi ulimsaidia Trump kushinda uchaguzi.
Saturday, March 4, 2017
JENGO LA REDIO YA GENGE LA DAESH, MOSUL LADHIBITIWA NA JESHI LA IRAQ
Habari kutoka mkoa wa Nainawa (Nineveh)
nchini Iraq zinaarifu kwamba jeshi la nchi hiyo limedhibiti jengo la
redio ya kundi la kigaidi na ukufurishaji la Daesh kwa jina la al-Bayan.
Jeshi la Iraq limekomboa eneo la Jawasaq katika pwani ya upande
wa kulia ya mji wa Mosul, sambamba na kubaini jengo na mnara wa
kurushia matangazo wa redio ya kundi hilo kwa jina la al-Bayan katika
mji huo. Kabla ya jeshi la Iraq kuwasili katika eneo hilo, genge hilo la
kigaidi lililichoma moto jengo la redio hiyo ili kupoteza ushahidi.
Hata hivyo jeshi la Iraq liliweza kunasa nyaraka muhimu katika nyumba
iliyokuwa karibu na jengo la redio hiyo ambazo zinajumuisha ripoti
muhimu za kiintelijensia za timu yote ya kundi hilo.
Itafahamika kuwa, redio hiyo ya kundi la Daesh (ISIS) ilikuwa
ikitangaza kwa lugha tano tofauti na kutoa matangazo ya kuwataka raia
kutekeleza operesheni za kigaidi. Kusambaratishwa redio hiyo kunatajwa
kuwa pigo jingine kubwa dhidi ya genge hilo linalopata himaya kutoka
Marekani, Israel, Saudia na baadhi ya za Kiarabu na Magharibi.
Wakati huo huo kitengo cha intelijensia katika jeshi la Iraq
kimetangaza habari ya kuuawa Abu Abdur-Rahman al-Answar, kiongozi wa
genge la kigaidi kwa jina la Jundul-Khilafah lenye mafungamano na kundi
la Daesh huko magharibi mwa mji wa Mosul. Kwa mujibu wa ripoti hiyo
gaidi huyo mwenye uraia wa Saudia ameuawa katika shambulio la anga akiwa
pamoja na viongozi wengine sita wa kundi hilo.
Jeshi la Iraq lilmetanga kuwa, kundi la Daesh (ISIS) limekuwa
likitumia silaha zenye gesi ya sumu katika kulizuia jeshi hilo kusonga
mbele katika maeneo yaliyosalia ya mji huo wa Mosul.
MAELFU WAKIMBIA MAPIGANO MAKALI SYRIA
Maelfu ya raia wa Syria wameyakimbia mapigano makali
kati ya vikosi vya serikali vinayoungwa mkono na Russia na wapiganaji
wa jihadi wa kundi lilalojiita Dola la Kiislamu wiki moja iliopita.
Vikosi vya serikali ya Syria vikisaidiwa na mashambulizi ya anga na
mizinga ya Russia vimeendesha mapambano makali dhidi ya kundi la Dola la
Kiislamu na kuviteka takriban vijiji 80 viliokuwa kwenye mikono ya
wapiganaji hao wa jihadi tokea katikati ya mwezi wa Januari.
Kwa
mujibu wa shirika la uangalizi wa haki za binaadamu nchini Syria lengo
la mashambulizi ya vikosi vya serikali ni kuuteka mji wa Kahafsah
unaoshikiliwa na kundi la IS mji ambao una kituo kikuu chenye kusambaza
maji kwa mji wa Allepo.
Wakaazi katika mji wa Allepo ambao ni mji
wa pili kwa ukubwa nchini Syria wamekuwa hawapati huduma ya maji kwa
siku 47 baada ya wapiganaji wa jihadi kukata usambazaji wa maji kwa mji
huo.Mapigano hayo katika kipindi cha wiki moja yamesababisha wimbi la
zaidi ya raia 30,000 kukimbia wengi wao wakiwa ni wanawake na watoto.
Wengi wakimbilia mji wa Manbij
Mkuu
wa shirika hilo Rami Abdel-Rahman amesema wengi ya watu waliokimbia
mapigano hayo wamekwenda kwenye maeneo karibu na mji wa Manbij
unaodhibitiwa na vijkosi vya (SDF) washirika wa wapiganaji wa Kikudi na
Waarabu wanaoungwa mkono na Marekani ambayo pia inapambana na kundi hilo
la IS.
Wengi wao wameshuhudiwa wakielekea katika mji huo kwa
kutumia piki piki,mabasi madogo na magari na wengi wao wameonekana kuwa
wachovu wakiwa katika misururu kwenye kituo cha ukaguzi kwa jili ya
kupekuliwa na kupata ruhusa ya kuingia.
Ibrahim al-Quftan
mwenyekiti mwenza wa mamlaka ya kiraia ya mji wa Manbij ameliambia
shirika la habari la AFP kwamba takriban watu 40,000 wamewasili katika
mji huo katika siku za hivi karibuni.Ameongeza kusema idadi hiyo ya watu
waliopotezewa makaazi inaendelea kuongezeka kutokana na mapigano kati
ya majeshi ya serikali ya Syria na kundi la Daesh kama
linavyotambulikana kwa Kiarabu (Dola la Kiislam).
Mji waemewa na wimbi jipya la waliopoteza makaazi
Na
kwa mujibu wa Abdel Rahman wa shirika la haki za binaadamu nchini Syria
mji huo wa Manbij tayari unawapa hifadhi maelfu ya watu waliopotezewa
makaazi ambao waliyakimbia mapigano yaliyopita katika eneo hilo na
wanaishi katika mazingira magumu.Amesema hali hiyo itafanya iwe vigumu
kwa mamlaka ya mji huo kukaribisha wimbi jipya la watu waliopotezewa
makaazi kutokana na kutokuwa na uwezo wa kushughulikia mahitaji yao ya
msingi.
Vita vya wenyewe kwa wenyewe vilianza nchini Syria hapo
mwezi wa Machi mwaka 2011 zaidi ya nusu ya idadi ya watu wake kabla ya
vita hivyo kuanza wamelazimika kuyakimbia makaazi yao.Mkoa wa kaskazini
wa Aleppo una maelfu ya Wasyria waliopotezewa makaazi wengi wao wakiwa
katika makambi na mpaka na Uturuki.
Zaidi ya watu 310,000
wameuwawa tokea mzozo huo wa Syria ulipoanza kwa maandamano ya kupinga
utawala wa Rais Bashar al-Assad lakini juhudi za kimataifa za kukomesha
mzozo hadi sasa zimeshindwa.
Sunday, February 26, 2017
RAIS YOWERI MUSEVENI AMALIZA ZIARA YAKE YA SIKU MBILI NA KUREJEA NCHINI KWAKE

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpokea
Mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni mara baada ya kuwasili
katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kwa
ajili ya kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake
ya siku mbili hapa nchini.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka ma kurejea nchini kwake.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza
na mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni katika Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Terminal 1 kabla ya kuondoka ma kurejea nchini kwake.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni wakati nyimbo za
Mataifa mawili zilipokuwa zikipigwa katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa
wa Julius Nyerere Terminal 1.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na
Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa
wakifurahia jambo wakati walipokwenda kumsindikiza Rais wa Uganda
Yoweri Kaguta Museveni katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere Terminal 1.

Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
mgeni wake Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla hajapanda ndege
na kurejea nchini kwake Uganda mara baada ya kumaliza ziara yake hapa
nchini.

Makamu
wa Rais Samia Suluhu Hassan akiagana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni kabla hajapanda ndege na kurejea nchini kwake Uganda mara baada
ya kumaliza ziara yake hapa nchini.

Mmoja wa Mtumbuizaji Uwanjani hapo akionesha umahiri wake wa kupuliza Tarumbeta.

Benderea za Matifa mawili ya Uganda na Tanzania zikipepea Uwanjani hapo. (PICHA NA IKULU)
RAIS MUSEVENI ATEMBELEA VIWANDA VYA BAKRESA JIJINI DAR ES SALAA LEO, AWAKARIBISHA WATANZANIA KUWEKEZA NCHINI UGANDA

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw.
Salim Aziz akimkabidhi zawadi Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta
Museveni baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa
Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.

Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akifurahia zawadi aliyopewa na
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz
(wapili kulia) mara baada ya kumaliza ziara katika viwanda vya Kuzalisha
Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda
cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia
kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Dkt. Augustine Mahiga.

Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya
maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha
Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda
cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia
kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).

Waziri
wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akifafanua jambo
mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga
wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda
cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia
ni Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim
Aziz.

Rais
wa Uganda Mhe.Yoweri Museveni(wapili kushoto) akiulizia jambo wakati wa
ziara yake katika viwanda vya Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo
Vingunguti jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kushoto ni Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz, Mkurugenzi wa
Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Hussein Sufiani na Katibu
Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji Dkt. Adelhelm Meru.

Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akishukuru kwa kupewa zawadi ya
maboksi ya Juisi za Azam mara baada ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha
Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda
cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. Kulia
kwake ni Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki
Balozi Dkt. Augustine Mahiga na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la
Makampuni ya Bakhresa Bw. Salim Aziz (kulia).

Mkurugenzi
wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akifafanua jambo mbele
ya waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa Ziara ya Rais wa
Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa
Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.

Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni(mweneye kofia) akiwa katika picha
ya pamoja na menejimenti ya Kundi la Makampuni ya Bakhresa mara baada
ya kumaliza ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano
Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha
Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.
Picha zote na: Frank Shija – MAELEZO.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa Bw.
Salim Aziz akimtambulisha Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni
kwa wafanyakazi wa alipofanya ziara katika viwanda vya Kuzalisha Unga wa
Ngano Cha Bakhresa Food Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo. 

Mkurugenzi
wa Mahusiano wa Kundi la Makampuni ya Bakhresa akimwelezea jambo Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni kwa wafanyakazi wa alipofanya
ziara katika Kiwanda cha Kuzalisha Unga wa Ngano Cha Bakhresa Food
Products kilichopo Buguruni na Kiwanda cha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.

Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni akiwasili katika Kiwanda cha
Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti Jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni
Afisa Mtendaji Mkuu wa Kundi la Kampuni za Bakhresa Bw. Salim Aziz.

Rais
wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akiangalia namna Juisi ya Azam
inavyotengenezwa alipofanya ziara katika Kiwanda hicho leo Jijini Dar es
Saalam. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe.Charles
Mwijage.

Baadhi ya wafanyakazi wa Kundi la Makampuni ya
Bakhresa wakifurahia ugeni wa Rais wa Uganda Mhe. Yoweri
Museveni(hayupo pichani) wakati wa ziara yake katika viwanda vya
Kuzalisha Juisi cha Azam kilichopo Vingunguti jijini Dar es Salaam leo.
MAZOEZI YA KIJESHI YA IRAN YANA UJUMBE WA AMANI
Kamanda wa Jeshi la Majini la Jamhuri ya
Kiislamu ya Iran amesema lengo la mazoezi ya majini ya Wilayat 95 ni
kutuma ujumbe wa amani na urafiki kwa nchi za eneo sambamba na kuinua
kiwango cha kujihami Iran.
Admeri Habibullah Sayyari Kamanda wa Jeshi la Majini la Iran
aliyasema hayo Jumamosi usiku katika mahojiano na Kanali ya Pili ya
Televisheni ya Iran. Amesema awamu ya mwisho ya mazoezi ya kijeshi
yaliyopewa jina la "Wilayat 95" yanaanza leo Jumapili na kuongeza kuwa,
upana wa eneo la mazoezi ni karibu kilomita mraba milioni mbili kuanzia
Lango Bahari la Hormoz kuelekea Bahari ya Oman hadi Kaskazini mwa
Bahari ya Hindi yapata daraja 10 kutoka mstari wa ikweta.
Admeri Sayyari amesema, kati ya malengo ya mazoezi hayo ni kuwapa
wanajeshi vijana uzoefu wa kikazi na kufanyia majaribio silaha mbali
mbali. Aidha ametaja lengo jingine la luteka hiyo kuwa ni kudumisha
amani katika eneo na kukabiliana na ugaidi pamoja na uharamia na
kuongeza kuwa: "Hadi sasa misafara ya meli za kivita za Iran imezisaidia
meli za nchi 25 duniani zikiwemo za Ufaransa, Uingereza na Marekani
katika kukabiliana na maharamia.
Admeri Sayyari amesema tokea mwaka 2008 hadi sasa, manowari za Iran
zimesindikiza meli za mafuta na za kibiashara zipatazo 3,850 katika
eneo la Bahari ya Hindi na Babul Mandab.
Admeri Sayyari amesema Iran ina uhusiano mzuri na nchi zote zenye
mipaka katika Bahari ya Hindi na Bahari ya Kaspi na kuongeza kuwa, mwaka
2018 Iran itakuwa mwenyeji wa makamanda wa majeshi ya majini ya nchi
zinazopakana na Bahari ya Hindi.
UN YATAKA UCHAGUZI UFANYIKE KUHUSU MAUAJI KASAI, DRC
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limetoa
taarifa likilaani vikali matukio ya utumiaji mabavu yaliyotokea katika
miezi ya hivi karibuni huko Kasai, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, na
kuihimiza serikali ya nchi hiyo kuchunguza mara moja matukio hayo.
Katika taarifa, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa
limeashiria ghasia katika miezi ya hivi karibuni huko Kasai na
kutokana na hali hiyo, wajumbe wa Baraza hilo wamesema wana hofu
kutokana na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kibinadamu za kimataifa
kukiwemo wanamgambo kutumikisha watoto vitani na jeshi la serikali kuua
raia.
Wamesema vitendo vyote hivyo vinaweza kuwa uhalifu wa kivita chini ya
sheria za kimataifa hivyo wametaka serikali iwajibike kulinda raia na
ijizuie kutumia nguvu za kijeshi kupita kiasi.
Wameitaka serikali kufanya uchunguzi usioegemea upande wowote na
wahusika wafikishwe mbele ya sheria huku wakisema kuwa ujumbe wa umoja
huo DRC, MONUSCO utakuwa tayari kusaidia iwapo utaombwa kufanya hivyo.
Kuhusu uchaguzi, wajumbe hao wamesisitiza umuhimu wa serikali ya DRC
na wadau wa kitaifa kuchukua hatua zote muhimu za kuandaa uchaguzi huo
bila kuchelewa na kuhakikisha mazingira ni salama kwa uchaguzi huru na
wa haki.
Wametoa wito kwa wadau wa maendeleo wa DRC kusaidia ili kufanikisha
uchaguzi huku wakisema wako tayari kufanikisha utekelezaji wa
makubaliano ya tarehe 31 mwezi Disemba mwaka jana yanayohusisha pia
uchaguzi.
Siku chache zilizopita, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa
Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein aliitaka serikali ya Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo kuchukua hatua za haraka kusitisha ukiukwaji
mkubwa wa haki za binadamu, ikiwa ni pamoja na mauaji ya raia
yanayofanywa na jeshi la nchi hiyo. Alisema kuna habari za kuaminika na
madai ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu katika eneo la Kasai ya
Kati na Mashariki na jimbo la lomami, huku kukiwa na kuzorota kwa kasi
hali ya usalama na watu wakilengwa na askari kwa madai ya kuwa na
uhusiano na wanamgambo wa ndani.
Subscribe to:
Posts (Atom)