Tuesday, January 31, 2017

RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA MARAIS MBALIMBALI WA AFRIKA KATIKA MAKAO MAKUU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) MJINI ADDIS ABABA ETHIOPIA

Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kuwasili kwa ajili ya mazungumzo katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya katika Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi akimkaribisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kwa ajili ya mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi mara baada ya kumaliza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za Makao Makuu ya Umoja wa Afrika (AU) mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoka kwenye mazungumzo yake pamoja na Rais wa Misri Abdel Fattah El Sisi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Akinwumi Adesina mara baada ya kumaliza mazungumzo yao mjini Addis Ababa nchini Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni kabla ya kuanza mazungumzo yao rasmi katika moja ya Ofisi za AU mjini Addis Ababa Ethiopia.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn wakati akitoka kwenye mkutano wa AU mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. 


PICHA NA IKULU

AU: AFRIKA IKO TAYARI KUPOKEA WAKIMBIZI BAADA YA USKUFUNGA MIPAKA YAKE

Umoja wa Afrika umesema nchi za Afrika ziko tayari kupokea wakimbizi baada ya Marekani kupasisha sheria tata ya kibaguzi dhidi ya wakimbizi.
Akizungumza pambizoni mwa mkutano wa AU unaomalizika leo mjini Addis Ababa, Ethiopia, Smail Chergui, Kamishna Mkuu wa Masuala ya Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika amesema kuwa, bara la Afrika linafaa kuwa mfano mzuri wa kuigwa duniani kwa kuendelea kuwapokea wakimbizi na wahamiaji, baada ya Marekani kutangaza kuwa itafunga mipaka yake kuzuia wakimbizi na wahamiaji kuingia nchini humo.
Ameongeza kuwa, historia inaonyesha kuwa nchi za Kiafrika zimekuwa zikiwapokea wakimbizi kwa moyo mkunjufu huku akitoa mfano wa Kenya, ambayo ina kambi kubwa zaidi ya wakimbizi duniani ya Dadaab.
Wakimbizi wa Iraq
Chergui amesema vikosi vya kieneo vinapigana kufa kupona kuyatokomeza makundi ya kigaidi kama al-Shabaab na Boko Haram, hivyo haingii akilini Marekani kutangaza kuwafungia nje wakimbizi kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi.
Smail Chergui, Kamishna Mkuu wa Masuala ya Amani na Usalama wa Umoja wa Afrika amesema kuwa, Marekani inafaa kutilia maanani wajibu wake wa kimataifa inapochukua uamuzi wowote wa kibaguzi na ambao unaweza kuhatarisha zaidi maisha ya wakimbizi.
Mwenyekiti anayeondoka wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma hapo jana alikosoa mikakati ya kibaguzi inayochukuliwa na serikali ya Rais Donald Trump wa Marekani kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi. 

Monday, January 30, 2017

CHINA: TAHADHARI YA KUTOKEA VITA NA MAREKANI SIO MANENO TU BALI NI KWELI HALISI

Viongozi wa China wamesema kuwa, indhari ya kutokea vita kati ya nchi hiyo na Marekani katika kipindi cha Rais Donald Trump, sio madai pekee, bali ni ukweli halisi.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu katika jeshi la China ambaye hakutaka kutaja jina lake sambamba na kusema maneno hayo ameongeza kuwa, katika kujiandaa na vita na Marekani, jeshi la nchi hiyo limeweka mfumo wa ulinzi wa makombora katika bahari ya kusini na mashariki mwa China, kwa ajili ya ulinzi wa Peninsula ya Korea. Afisa huyo wa jeshi la China amesisitiza kuwa, Beijing imeingia katika awamu mpya ya kujiimarisha kiulinzi kutokana na hatari inayolikabili eneo la kusini mashariki mwa Asia.
Jeshi la Uchina
China imechukua hatua hizo kutokana na matamshi ya uhasama ya rais mpya wa Marekani Donald Trump dhidi ya nchi hiyo. Hivi karibuni pia jeshi la China lilitangaza kuwa, kuendelea kuwa mbaya hali ya mambo kuhusiana na usalama wa bahari ya eneo, machafuko katika eneo la Asia na Bahari ya Pasifiki na kadhalika misimamo tata ya rais huyo mpya wa Marekani, inailazimu kujiandaa kuingia katika vita tarajiwa na Marekani kuliko wakati mwingine wowote ule.
Jeshi la Uchina likiwa katika maandalizi
Ripoti hiyo ya jeshi la China ilifafanua kuwa, msimamo wa Washington wa kuweka ngao ya makombora ya THAD nchini Korea Kusini, kuongeza idadi ya askari wake katika maeneo ya mashariki na kusini mwa bahari za Uchina na kadhalika kuanzisha mlingano mpya wa kijeshi barani Asia, ni siasa ambazo zinaweza kuwasha moto wa vita wakati wowote. Mwezi Disemba mwaka jana, Donald Trump alitangaza kuwa, Washington haitafungamana na siasa za 'China Moja' kuhusiana na uhusiano wa nchi yake na Taiwan, suala ambalo lililalamikiwa na Beijing.
Makomando wa jeshi la China wakiwa katika mafunzo
Hii ni kwa kuwa mara kadhaa Beijing imekuwa ikitangaza kuwa, siasa za 'China Moja' ni suala lisilo na mjadala huku ikiitaka Washington kuangalia upya siasa zake kuhusiana na suala hilo.

KUONGEZEKA CHUKI DHIDI YA WAISLAMU AMERIKA KASKAZINI

Baada ya kuongezeka hisia za chuki na uadui dhidi ya Waislamu huko Amerika Kaskazini hususan baada ya kuingia madarakani Rais Donald Trump nchini Marekani, hivi sasa matokeo mabaya ya jambo hilo yameanza kuonekana.
Jana Jumatatu, maafisa wa Canada walitangaza habari ya kushambuliwa msikiti mmoja na kuuliwa Waislamu watano huko Quebec na kujeruhiwa wengine kadhaa. Waislamu 40 walikuwemo msikitini humo wakati watu watatu wenye chuki za kidini walipowashambulia kwa risasi. Polisi wa Quebec wamesema. watu wawili kati ya watatu walioushambulia kwa risasi msikiti huo, wametiwa mbaroni.
Komesha chuki dhidi ya Waislamu
Tukio hilo linaonesha ni kiasi gani propaganda mbaya dhidi ya Waislamu zilivyo na madhara kiasi kwamba zinaweza kusababisha mauaji ya Waislamu. Hivi sasa propaganda za chuki dhidi ya Waislamu zimeshika kasi zaidi nchini Marekani, lakini madhara ya propaganda hizo chafu yanaonekana hadi nje ya mipaka ya Marekani. Ikumbukwe kuwa propaganda za chuki dhidi ya Waislamu nchini Canada ni ndogo ikilinganishwa na Marekani. Kabla ya hapo pia msikiti wa Ranchview katika mji wa Calgary wa jimbo la Alberta huko Canada ulishambuliwa na watu wenye chuki za kidini. Shambulio la jana Jumatatu dhidi ya Waislamu wa Canada limefanyika katika hali ambayo wiki za hivi karibuni, misikiti ya nchi hiyo ilifungua milango yake kwa ajili ya kuwahudumia watu wasio na makazi nchini humo.
Nukta ya kuzingatiwa hapa ni namna shambulio hilo lilivyosadifiana kwa kiasi fulani na amri iliyotolewa na Rais wa Marekani Donald Trump ya kuwazuia raia wa nchi saba za Kiislamu kuingia Marekani. Hatua hiyo ya serikali ya Marekani inakinzana kikamilifu na sehria za kimataifa. Hatua hiyo imelalamikiwa vikali kote ulimwenguni. Waendesha Mashtaka Wakuu wa majimbo 16 ya Marekani yakiwemo ya California, New York na Pennsylvania walitoa tamko siku ya Jumapili na kulaani amri ya Trump ya kuwapiga marufuku raia wa nchi hizo za Kiislamu kuingia Marekani.
Moja ya misikiti ya Waislamu wa Canada mjini Calgary katika jimbo la Alberta

Vitendo vya chuki na uadui dhidi ya Waislamu vimeongezeka sana huko Amerika Kaskazini tangu baada ya kutokea shambulio la kigaidi katika mji wa San Bernardino wa jimbo la California huko Marekani mwezi Disemba 2015. Vile vile mahambulizi ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni barani Ulaya yamezidi kuwapa kisingizio maadui wa Uislamu kuwasakama Waislamu na kudhihirisha waziwazi chuki zao dhidi ya wafuasi wa dini hiyo tukufu ya Mwenyezi Mungu. Wakati wa kampeni za uchaguzi nchini Marekani, Trump alitangaza kuwa atapiga marufuku kuingia Waislamu nchini humo kama njia ya kukabiliana na ugaidi. Matamshi hayo ya chuki yalilaaniwa vikali katika pembe mbalimbali za dunia, ndani na nje ya Marekani. Hata hivyo, rais huyo mwenye chuki za kidini hakujali malalamiko hayo makubwa ya walimwengu na ametoa amri ya kuzuia kijeuri na kinyama raia wa nchi saba za Waislamu kuingia nchini humo.
Waislamu wa Marekani wakilalamikia unyanyasaji
Hivi sasa kumejitokeza wasiwasi mkubwa wa kuongezeka vitendo vya kikatili na vya chuki za kidini dhidi ya Waislamu wasio na hatia. Shambulio la kikatili lililofanywa dhidi ya Waislamu tena nchini Canada ambako hakuna historia ya mashambulizi makali kama hayo dhidi ya Waislamu linaonesha kuwa wingu jeusi la chuki na uadui wa kidini dhidi ya Waislamu limezidi kutanda huko Amerika Kaskazini. Hali hiyo mbaya si tu ni hatari kubwa kwa usalama wa kikazi na kimakazi wa Waislamu wa nchini Marekani na Canada, lakini pia Waislamu wa nchi hizo hivi sasa wana hofu ya kupoteza roho zao hata wanapotembea mitaani na wanapokuwa kwenye nyumba zao za ibada, licha ya mapenzi makubwa wanayowaonesha wafuasi wa dini nyinginezo na kuwathibitishia kuwa propaganda zote dhidi yao zinatokana tu na chuki za kidini za maadui wa Uislamu.  

JESHI LA YEMEN LAANGAMIZA MELI YA MIZIGO YA SAUDIA, RIYADH YAKIRI

Jeshi la Yemen Jumatatu ya jana liliangamiza meli ya mizinga ya Saudia na kusababisha makumi ya askari wa nchi hiyo vamizi kuangamizwa na wengine kujeruhiwa.
Sambamba na Saudia kukiri juu ya habari hiyo imedai kuwa, katika shambulizi la jeshi la Yemen dhidi ya meli yake ya mizinga katika pwani ya mkoa wa Al Hudaydah, askari wake wawili waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa. Wakati huo huo jeshi la Saudia limeshambulia mji mdogo wa pwani wa Al Mukha kusini mwa mkoa wa Taiz na kusababisha makumi ya raia kuuawa shahidi na wengine wengi kujeruhiwa.
Mfalme wa Saudia anayetekeleza jinai na mauaji dhidi ya raia madhlumu wa Yemen
Aidha shambulizi hilo lilililenga daraja la Irfan mjini humo. Kwingineko jeshi la Yemen kwa kushirikiana na harakati ya wananchi ya Answarullah imeangamiza askari vibaraka wa Saudia waliokuwa wanakimbia uwanja wa mapigano baada ya kuzidiwa. Kwa mujibu wa habari hiyo askari kadhaa vibaraka wa Aal-Saud wameangamizwa katika mkoa wa Taiz kusini magharibi mwa Yemen.
Sehemu ya jinai za utawala wa kidikteta wa Aal-Saud huko Yemen
Hii ni katika hali ambayo kwa mara nyingine jeshi la Yemen limezilenga kambi za jeshi la Saudia za Jizan na kuisababisha nchi hiyo kibaraka wa Marekani na Israel hasara ya maafa na uharibifu. Kama ambavyo jeshi hilo la Yemen na harakati ya Answarullah limeshambulia kwa makombora mengi kambi ya jeshi ya al-Makhruq iliyopo eneo la Quwah mkoani Najran na kuangamiza askari kadhaa.

WATU WANANE WAUAWA KWA KUPIGWA RISASI MSIKITINI QUEBEC, CANADA

Quebec City
Polisi wamekiri kunao watu wamefariki lakini hawajataja idadi
Watu wanne wameuawa kwenye ufyatulianaji wa risasi katika msikiti mmoja mjini Quebec, Canada.
Ufyatulianaji wa risasi ulitokea katika Kituo cha Kitamaduni cha Kiislamu cha Quebec Jumapili usiku, polisi wamesema.
Kituo hicho kimepakia kwenye ukurasa wake wa Facebook video inayoonesha polisi wakiwa nje ya kitu hicho. Video hiyo imeambatana na ujumbe kwamba "baadhi wamefariki".
Polisi wamesema watu wawili wamekamatwa, lakini hawajatangaza idadi kamili ya waliofariki au kujeruhiwa.
Mtu aliyeshuhudia ameambia shirika la habari la Reuters kwamba watu hadi watatu waliokuwa na silaha wamehusika.
Shirika hilo la habari pia limesema maafisa wa usalama waliokuwa na silaha kali wameonekana wakiingia kwenye msikiti huo.
Gazeti la Le Soleil linasema limepata taarifa kwamba mmoja wa washukiwa ni kijana wa miaka 27 mwenye "jina la asili ya Quebec", na alikuwa na bunduki aina ya AK-47.
Ufyatuaji huo wa risasi umetokea katika msikiti ulio kwenye barabara ya Sainte-Foy, moja ya misikiti miwili inayoendeshwa na kituo hicho cha utamaduni wa Kiislamu.
Shambulio lilitekelezwa wakati wa sala ya jioni.
Polisi wamewakamata watu wawili
Polisi wamewakamata watu wawili
Rais wa msikiti huo Mohamed Yangui, ambaye hakuwa ndani ya msikiti wakati wa shambulio, ameambia Reuters kwamba hajafahamu kufikia sasa idadi ya waliojeruhiwa ingawa wamepelekwa hospitali mbalimbali Quebec.
"Nini kinatendeka hapa? Huu ni unyama," amesema.
Juni mwaka jana, kulipatikana karibu na mlango wa msikiti huo kichwa cha nguruwe kilichokuwa kimefungwa vizuri kama zawadi na kuandikwa "bonne appetit". Waislamu hawali nguruwe.
Kichwa
Kituo hicho kilisema zawadi hiyo ilikuwa "ishara ya chuki"
Waziri Mkuu wa Justin Trudeau ameandika kwenye Twitter kwa Kiingereza na Kifaransa na kusema, "Usiku huu, raia wa Canada wanaomboleza waliouawa kwenye shambulio hili la woga katika msikiti mmoja Quebec. Fikira zangu ni kwa waathiriwa na jamaa zao.

Thursday, January 26, 2017

RAIS BARROW AREJEA GAMBIA, ATAKA KIKAO CHA KIENEO KIBAKIE NCHINI MIEZI 6

Rais mpya wa Gambia Adama Barrow amerejea nchini kwake leo Alkhamisi akitokea nchi jirani ya Senegal, ambayo alilazimika kuigeuza kimbilio lake tangu Januari 15, akihofia usalama wake.
Mohammed Ibn Chambas, afisa wa Umoja wa Mataifa katika eneo la magharibi mwa Afrika amewaambia waandishi wa habari nchini Senegal kuwa, Barrow ameomba kikosi cha askari wa kieneo kisalie nchini humo kwa miezi sita zaidi, hadi mambo yatakapotengamaa. Afisa huyo wa UN ameongeza kuwa, uamuzi wa mwisho wa ombi la Rais Barrow utatolewa na Jumuiya ya Kiuchumi ya Magharibi mwa Afrika ECOWAS.
Rais Barrow akiapishwa katika ubalozi wa Gambia nchini Senegal wiki jana
Msemaji wa Barrow, Halifa Sallah amethibitisha kuwa, rais huyo mpya wa Senegal anaingia nchini leo na kwamba sherehe za kumpokea zitafanyika baadaye.
Rais Barrow anarejea Gambia baada ya kuondoka mtangulizi wake aliyeiongoza nchi hiyo ndogo ya magharibi mwa Afrika kwa miaka 22, Yahya Jammeh.
Jammeh ambaye yuko uhamishoni nchini Equatorial Guinea, anadaiwa kuondoka nchini Gambia na dola milioni 11 za Marekani kutoka hazina ya taifa, tuhuma ambazo kiongozi mpya wa taifa ameagiza zichunguzwe.
Yahya Jammeh akiondoka Banjul, Gambia
Wananchi wa Gambia wana matarajio mengi kutoka kwa uongozi wa Barrow. Tayari rais huyo mpya wa Gambia amemteua afisa wa zamani wa Umoja wa Mataifa, Fatoumata Tambajang kuwa makamu wake.

RAIS DK MAGUFULI MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI


Benjamin Sawe-Maelezo.
Rais John Magufuli anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Sheria nchini zitakazofanyika mwanzoni mwa mwezi ujao katika viwanja vya Mahakama jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam, Kaimu Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma amesema mahakama itawaelimisha wananchi jitihada mbalimbali ilizochukua zenye lengo la kuboresha huduma zake kupitia mpango mkakati wa miaka mitano inaoutekeleza katika kutoa haki kwa wakati na kuwezesha ukuaji wa uchumi.

Amesema kabla ya kilele cha maadhimisho hayo, mahakama itafanya matembezi maalum yatakayoongozwa na Rais Mstaafu Ali Hassan Mwinyi  na yataanzia Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuishia katika viwanja vya Mnazi mmoja.

Katika matembezi hayo Rais Mstaafu Mwinyi atazindua rasmi maadhimisho ya wiki ya elimu ya sheria ikiwa ni sehemu ya sherehe za kuelekea maadhimisho ya kilele cha siku ya sheria nchini.

Aidha ametoa rai kwa wananchi kutembelea sehemu zote zilizoandaliwa kwa ajili ya utoaji elimu ya sheria nchini kwa ajili ya kujifunza na kupata huduma mbalimbali za Kisheria.

Alizitaja huduma hizo ni pamoja na taratibu za ufunguaji mashauri katika ngazi mbalimbali za mahakama, taratibu za kesi za mirathi, taratibu za kesi za dhamana, taratibu za rufaa, ndoa na talaka, taratibu za kupokea na kushughulikia malalamiko na Msaada wa Kisheria.

Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini hufanyika kila mwaka mwanzoni mwa mwezi wa pili na mwaka huu yamebeba ujumbe wa Umuhimu wa Utoaji Haki kwa Wakati Kuwezesha Ukuaji wa Uchumi

SYRIA, IRAN CALL FOR NATIONWIDE TRUCE CONSOLIDATION

Syrian President Bashar al-Assad (R) and Iranian parliament speaker's special advisor on international affairs, Hossein Amir-Abdollahian, meet in Damascus on January 26, 2016. (Photo by SANA news agency)
Syrian President Bashar al-Assad (R) and Iranian parliament speaker's special advisor on international affairs, Hossein Amir-Abdollahian, meet in Damascus on January 26, 2016. (Photo by SANA news agency)
Damascus and Tehran have reaffirmed their support for a country-wide cessation of hostilities that has been largely holding in Syria for almost a month now.
During a meeting in Damascus on Thursday, Syrian President Bashar al-Assad and Iranian parliament speaker’s special advisor on international affairs, Hossein Amir-Abdollahian, said a successful ceasefire would pave the way for the restoration of permanent peace and stability to Syria.
Under the truce, the anti-terror fight will continue and conditions will be prepared for launching intra-Syrian dialogue, enabling the nation to decide its future, the two sides stressed.
Mediated by Russia and Turkey with the support of Iran, the Syria ceasefire took effect on December 30, 2016, following an agreement between Syria’s warring parties.
The truce is the first of its kind that has been largely holding in Syria for nearly a month. Earlier attempts by the US to broker such a long-lasting ceasefire had failed.
Read more
During the Thursday talks, the Syrian leader hailed Iran’s constructive role in backing the Syrian people in the face of terrorism as well as in efforts to find a peaceful solution to the Syria crisis.
Syrian President Bashar al-Assad (C-R) and Iranian parliament speaker's special advisor on international affairs, Hossein Amir-Abdollahian, meet in Damascus on January 26, 2016. (Photo by IRIB)
Amir-Abdollahian, for his part, said the Islamic Republic’s support for Syria is rooted in the strategic relations between the two nations.
He further empathized that Tehran believes terrorism in Syria poses an imminent threat to the entire region.
Earlier on Thursday, the Iranian official met with Syrian Foreign Minister Walid al-Muallem to discuss bilateral ties and the latest developments in the Arab country.
They underlined the need for continued the trilateral Syrian-Iranian-Russian cooperation to settle the Syria conflict based on the outcome of the latest round of the peace talks held in Kazakhstan earlier this week.
Read more
On Wednesday, Amir-Abdollahian sat down with Syria’s Parliament Speaker Hadiyeh Khalaf Abbas.
Iran has been offering military advisory support to the Syrian military, which has been battling foreign-backed militancy since 2011.

POLISI NIGERIA WAWAFYATULIA MABOMU YA KUTOWA MACHOZI WAFUASI WA SHEIKH ZAKZAKY

Maafisa usalama nchini Nigeria wamewafyatulia mabomu ya kutoa machozi wafuasi wa kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo, Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye anaendelea kuzuiliwa kinyume cha sheria.
Shirika la habari la Press TV limeripoti kuwa, mamia ya wafuasi wa Sheikh Zakzaky hapo jana walifyatuliwa mabomu ya kutoa machozi walipokuwa wakishiriki maandamano ya amani ya kuonyesha uungaji mkono wao kwa kiongozi wao, nje ya bunge la nchi hiyo katika mji mkuu Abuja.
Maafisa wa polisi wa Nigeria waliyavunja maandamano hayo ya amani kwa mabomu ya machozi, ambapo watu kadhaa walijeruhiwa. Waandamanaji hao ambao walikuwa wamebeba picha za Zakzaky na maberamu yenye ujumbe unaosema, "Muachieni huru Zakzaky" walisikika wakiikosoa vikali serikali ya Abuja kwa kuendelea kumzuilia Sheikh Zakzaky licha ya agizo la mahakama.
Maandamano ya amani Abuja ya kushinikiza kuachiwa huru Sheikh Zakzaky
Itakumbukwa kuwa Mahakama ya Shirikisho la Nigeria hivi karibuni ilitoa amri ya kuachiliwa huru Sheikh Ibrahim Zakzaky, lakini serikali ya Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo inavunja waziwazi amri hiyo ya mahakama kwa kukataa kumwachilia huru kiongozi huyo wa Harakati ya Kiislamu.
Umoja wa Ulaya na shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International ni baadhi ya taasisi za kimataifa zilizotoa taarifa zikiwataka viongozi wa Nigeria kuheshimu amri ya mahakama ya kumwachilia huru mara moja kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo.

MEXICO: HATUTALIPIA UKUTA WA DONALD TRUMP

Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico kushoto na mwenzake wa Marekani Donald Trump kulia
Rais Enrique Pena Nieto wa Mexico kushoto na mwenzake wa Marekani Donald Trump kulia
Mexico imesema kuwa haitalipia ukuta uliopendekezwa na rais wa Marekani Donald Trump ,kulingana na rais wa taifa hilo Enrique Pena Nieto ambaye ameshutumu mpango huo wa kujenga ukuta.
Hata hivyo rais huyo hakizungumzia kuhusu iwapo atafutilia mbali ziara yake ya Marekani ambapo anatarajiwa kukutana na rais Donald Trump.
Trump tayari amesaini agizo la urais la kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico na amesisitiza kuwa Mexico itailipa Marekani kwa ukuta huo.
Rais Pena Nieto aliambia taifa katika hotuba ya runinga kwamba :Nimesema tena na tena kwamba Mexico haitalipia ukuta huo.
''Ninajuta na kushutumu uamuzi huo wa marekani wa kutaka kuendelea kujenga ukuta ambao umetugawanya kwa miaka badala ya kutuunganisha''.
Lakini Nieto amesema kuwa urafiki kati ya Mexico na raia wa Marekani utadumu mbali na kutafuta suluhu kuhusu tatizo la wahamiaji.
Waziri wa maswala ya kigeni nchini Mexico Luis Videgaray ambaye yuko mjini Washington amesema kuwa rais huyo bado anaendelea kupima uwezekano wa ziara ya Marekani siku ya Jumanne lakini akaongezea kuwa mkutano huo bado utafanyika kufikia sasa.

Wednesday, January 25, 2017

WASOMALI 90 NA WAKENYA WAWILI WATIMULIWA MAREKANI

Raia takriban 90 wa Somalia na wawili wa Kenya wametimuliwa kutoka Marekani saa chache baada ya taarifa kuibuka kwamba Rais Donald Trump atakabiliana na watu wanaoishi nchini humo kinyume cha sheria.
Wote waliwasili katika uwanja wa kimataifa wa Jomo Kenyatta jijini Nairobi, lakini baadaye raia wa Somalia wakaendelea na safari hadi uwanja wa ndege wa Aden Abdulle mjini Mogadishu. Msemaji wa serikali ya Kenya Eric Kiraithe ameambia BBC kwamba ni kweli raia hao wamefukuzwa Marekani, ingawa hakusema iwapo hatua hiyo imetokana na msimamo wa Bw Trump.. "Ni watu 90 kulingana na habari ambazo tulipewa. Wakati unaondolewa nchi fulani kurejeshwa kwenu, huwa unarejeshwa hadi kwenu," ameambia BBC. Kuhusu sababu iliyowafanya kufurushwa, Bw Kiraithe amesema: "Inategemea sheria za nchi ambayo walikuwa wamehamia (Marekani),"

Tuesday, January 24, 2017

ISRAEL PLANS 2,500 NEW SETTLEMENT HOMES IN OCCUPIED WEST BANK

By Ori Lewis
JERUSALEM (Reuters) - Israel announced plans on Tuesday for 2,500 more settlement homes in the occupied West Bank, the second such declaration since U.S. President Donald Trump took office signaling he would be less critical of such projects than his predecessor.
A statement from the Defence Ministry, which administers lands Israel captured in a 1967 war, said the move was meant to fulfill demand for new housing "to maintain regular daily life".
Most of the construction, it said, would be in existing settlement blocs that Israel intends to keep under any future peace agreement with the Palestinians. However, a breakdown provided by the prime minister's office showed large portions of the planned homes would be outside existing blocs.
About 350,000 settlers live in the West Bank and a further 200,000 in East Jerusalem, which Israel seized in the 1967 Middle East war. Beyond the major blocs, most of which are close to the border with Israel, there are more than 100 settlement outposts scattered across hilltops in the West Bank.
Nabil Abu Rdainah, a spokesman for Palestinian President Mahmoud Abbas, condemned the Israeli announcement and said it would have "consequences".
"The decision will hinder any attempt to restore security and stability, it will reinforce extremism and terrorism and will place obstacles in the path of any effort to start a peace process that will lead to security and peace," he said.
They want the West Bank and Gaza Strip, from which Israeli troops and settlers withdrew in 2005, for an independent state, with its capital in East Jerusalem.

Monday, January 23, 2017

WATU ZAIDI YA 19 WAPOTEZA MAISHA BAADA YA JIMBO LA GEORGIA KUKUMBWA NA KIMBUNGA, RAIS TRUMP ATUMA SALAM ZA RAMBIRAMBI

Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Wakazi wa mji wa Albany jimbo la Georgia wakiwa na hudhuni kubwa baada ya nyumba zao kubomolewa na kimbunga siku ya Jumapili Jan 22, 2017 na inasadikika watu zaidi ya 19 wamepoteza maisha na zaidi ya watu 23, wamejeruhiwa. Rais Donald Trump aliongea kwa simu ya Gavana wa jimbo hilo na kutuma salam za rambirambi na kutoa pole kwa wananchi wa jimbo hilo kwa kukumbwa na kimbunga hicho kilichoikumba mji huo kusini ya jimbo la Georgia inayopakana na sehemu ya kaskazini ya jimbo la Florida.
Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Sehemu iliyoharibiwa na kimbunga hicho.
Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Mmoja ya waathirika wa kimbunga akiwa kwenye majonzi mengi.

Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Nyumba ikiwa imeharibiwa vibaya na kimbunga.
Image result for tornado HIT GEORGIA JAN 22, 2017
Miti ikiwa imeanguka na paa likiwa limeuzuliwa na kimbunga kilichoikumba jimbo la Georgia.

Friday, January 20, 2017

JAMMEH ASEMA ATAONDOKA MADARAKANI

Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow
Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi na Adama Barrow
Kiongozi wa muda mrefu nchini Gambia Yahya Jammeh, anasema kuwa ataondoka madarakani baada ya kukataa kukubali kushindwa.
Katika tangazo kwenye runinga, Jammeh alisema kuwa hakuna haja ya hata tone moja la damu kumwagika.
Taangazo hilo linakuja saa kadha baada ya mazungumzo kati ya bwana Jammeh na wapatanishi wa Afrika Magharibi. Hata hivyo hakuna taarifa zaidi kuhusu yale yayoafikiwa.
Bwana Jammeh alishindwa kwenye uchaguzi wa mwezi Disemba na mrithi wake Adama Barrow tayari amesha apishwa.
Bwana Barrow amekuwa akiishi katika taifa jirani la Senegal kwa siku kadha.
Wanajeshi kutoka nchi za magharibi mwa Afrika ikiwemo Senegal wametumwa nchini Gambia wakitisha kumtimua bwana Jammeh madarakani.
Uamuzi wa bwana Jammeh kuondoka ulikuja kufuatia mazungumzo na marais wa Guinea na Mauritania.

BARROW: YAHYA JAMMEH AMEKUBALI KUONDOKA MADARAKANI GAMBIA

Rais Yahya Jammeh wa Gambia amekubali kuondoka madarakani kumpisha rais mpya Adama Barrow.
Kwa mujibu wa ripoti,  Jammeh anaondoka nchini humo kwenda kuishi uhamishoni, ingawa bado haijafahamika ni nchi gani ataelekea. Habari za kuondoka rais huyo aliyetawala Gambia kwa miaka 22 sasa zimetolewa na rais anayetambuliwa na jamii ya kimataifa Adama Barrow kupitia mtandao wake wa Twitter. Barrow ameeleza hayo baada ya mazungumzo ya saa kadha yaliyokusudia kumshawishi Yahya Jammeh kukubali matokeo ya uchaguzi wa tarehe Mosi Disemba mwaka jana.
Aliyekuwa rais wa Gambia Yahya Jammeh
Hii ni katika hali ambayo nchi kadhaa za Afrika Magharibi zimewatuma wanajeshi wao nchini Gambia na kutishia kumuondoa Jammeh madarakani kwa nguvu iwapo angekaidi amri ya kuachia madaraka kwa hiari. Barrow amekuwa nchini Senegal kwa takriban wiki moja sasa ambapo pia aliapishwa kuwa rais mpya wa Gambia katika ubalozi wa nchi hiyo mjini Dakar Alkhamisi iliyopita. Sasa Barrow anatambuliwa na jamii ya kimataifa kuwa kiongozi mpya wa Gambia.